Mwanaume usikubali kuuza nafasi yako uliyopewa na Mungu kama kichwa cha familia, hata umpende mwanamke kiasi gani nafasi yako ndio heshma yako

Mwanaume usikubali kuuza nafasi yako uliyopewa na Mungu kama kichwa cha familia, hata umpende mwanamke kiasi gani nafasi yako ndio heshma yako

mama D

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
19,981
Reaction score
35,581
Tangu ijumaa tarehe 15 January 2021 imekua siku mbaya sana kwa bwana Abdul Jamaa aliyekua akijulikana kama baba Nasibu au Mzee Dangote.
Hii issue ya mzee Abdul itapita lakini sisi kama jamii tuna jambo kubwa sana kujifunza haswa kwenye mahusiano na hata kwenye malezi.

Kwa wale waamini wa Mungu vitabu vitakatifu vinatoa miongozo mizuri kuhusu tunavyotakiwa kuishi, na hata wale wasioamini kwa Mungu miongozo hii ni muhimu kwani ndio sheria na taratibu za kudumisha amani na nidhamu kwenye jamii.

Mungu alimuumba mwanaume kwanza kabla ya mwanamke, na alifanya hivyo akijua umuhimu wake wa kuwa hapa duniani na uwezo wake wa kubeba majukumu. Mungu alipoona amekua mpweke alimpa mwanamke ili awe msaidizi wake. Na katika maandiko pamoja na mambo mengine maandiko yanaongelea wajibu na majukumu ya mwanaume na mwanamke.

Wanaume vaeni viatu vyenu, hata kama una mwanamke anaweza kufanya baadhi ya majukumu usibweteke sababu wanawake hufanya vitu wakiwa na mapenzi ila mapenzi yakiisha hubaki kuwa fedheha kwa mwanaume.

Tumemwona mzee Abdul alivyokwisha dhalilika na anavyoendelea kudhalilika na kuumia. Huyu mzee inawezekana kabisa kwenye ujana wake alisahau nafasi yake sababu ya mapenzi tuu aliyokua anapata, akasahau kwamba mambo yanaweza kubadilika.

Yeye anadai nasibu ni mwanae kabisa bila wasiwasi wowote lakini pia ukimsikiliza utagundua utakwamba hakuwahi kubeba majukumu yake ndio maana anakosa hata pa kusimama walau kuutetea utu wake tuu. Mambo yamemuwia magumu sababu hajawahi simama kwenye nafasi yake kama baba au mume kijamii wala kiimani

1.Hakuwahi kumuoa mama Nasib kwa kufuata taratibu zozote za anasema, za kiserikali au za kimila. Kwa maana ya taratibu huyu mwanamke hajawahi kuwa mke wake kitu ambacho kilipelekea kuzaa
~Hapakua na makubaliano

2.Mzee Abdul Jumaa kama mwanaume hakuwahi kumiliki makazi akamchukua mama Nasib na kuishi nae ndani kama familia. Anasema yeye alihamia nyumbani kwao mama nasib, nyumba aliyokua wanaishi wazazi wa mama nasib pamoja na ndugu zake wengine
~Kuishi ukweni hata kama umeoa ni fedheha kubwa sana kwa mwanaume. Sasa hapa huyu kijana wa zamani alikosea sana maana hata hakuwa ukweni, hakuwa ameoa wala kulipa mahari

3.Mzee Abdul anasema kisa cha kutengana ni kwamba mama Nasib alitoka akaenda kwa mwanaume mwingine hadi saa nane ya usiku akawa hajarudi
~Akufukuzae hakuambii toka. Hii familia walimchoka wakamuona mzigo sababu anaishi kwao, ndio maana mama nasib akawa na guts za kwenda huko anakosemekana kwenda ili jamaa aondoke

4.Baada ya kuondoka Mzee Abdul anasema hakuwahi kurudi wala kuwasliana na mama Nasib wala nasib hadi alipoanza kupa umaarufu
~Hii ni wazi kwamba mzee yalimfika hapaaa!!! Na kwakua hakuacha kitu (mke wala mtoto wa damu) haikua shida kwake kuwacancel na kuendelea na shughuli zake.... bila kujua kwamba na wao wamemcancel na kuendelea na mambo yao

Baada ya Nasib kupata umaarufu mzee Abdul alianza kurudi sababu anajua wazi nasib ameshakua maarufu na anatumia jina lake hakuna ambaye angeweza kumzuia... Mama nasib alivumilia sababu ya mwanae lakini anavyodai alikua akimwambia "wewe ulikataa majukumu....mtoto ungemtunza angekua wako..." Ila mzee Abdul aliendelea kukomaa na medias hadi yakatokea yaliyotokea.

Maskini hakujua wanawake wakibadilika wanabadilika jumla, hawajali aibu wala fedheha! Sasa mzee Abdul ataingia kwenye phase2 ya aibu kama DNA itafanyika japo yeye mwenyewe ameshagomea DNA kwa madai kwamba mtoto hagombewi!

Wanaume wanawake ni watu wazuri na wapole sana ila mnapoishi msiishie kuishi kama marafiki tuu. Waongozeni wanawake zenu kwenye imani, mila na desturi ili heshma na upendo viwe nguzo ya familia.
Binadamu sisi tuko kama tulivyo, jitahidini kuishi na sisi mkiwa wanaume maobeba majukumu yenu na mamlaka ndani ya mahusiano, familia na jamii. Mkilegea ndio tunaishia kutengeneza familia ambazo majukumu ya familia anabeba mama halafu akishayabeba yote anachukua na maamuzi nyumba inakua shubiri.

Salim Nyange RIP na mwanae Nasib Salim Nyange
MOND NA BABA AKE, JE WANAFANANA__  _ HUYU NDIO BABA YAKE HALISI WA @diamondplatn ( 778 X 750 ).jpg
 
Mi naona huyo Abduli anastahili yanayomtokea, diamond mwenyewe alishagasema huyo Abduli alimkataa mkavu live bila chenga, anaanza kutafuta huruma sababu ya umaarufu aliopata tu hana lolote,

Mwanamke akipenda anapenda kweli na akiacha anaacha
Alimtelekeza, akadanga akajiuza ili kumlea mwanae, mtoto kafanikiwa tumuache afaidi, tunaona matusi kwa singo mama's humu na kwenye jamii, si ajabu hata huyo Abduli alikuwa sehemu ya walionanga na kumdhihaki,
japo mama nasibu ana tabia za kiswahili ila km hizo drama zinampa ahueni na raha Basi wacha afaidi mali na umaarufu wa mwanae
 
Hakuna mahali huyu Abdul alisimama kama mwanaume au baba
Kwanza kuishi kwa wakwe ambao hata mahari hujalipa ni aibu kubwa sana
 
Umeongea point ila umeegemea one side!!...
Namlaumu mama Nasib kwa kumkubalia Abdul kuja kumnanihino nyumbani kwao. Huo ni ujinga na dharau kubwa sana kwao kama familia na hata kwa huyo Abdul japo hadi leo haoni kama hilo ni tatizo
 
Hakuna mahali huyu Abdul alisimama kama mwanaume au baba
Kwanza kuishi kwa wakwe ambao hata mahari hujalipa ni aibu kubwa sana
Anavuna alichopanda, atajiju mi simuhurumii Kwanza Sandra kamsitiri kwa muda, mwanae anapewa laana mtandaoni kwa kumtelekeza baba ambae si baba mzazi wala mlezi, kisa jina tu,, mama mtu kaona isiwe shida kaamua kusema hadharani ili kumpunguzia mwanae laana za kimtandao
 
Ukikutana na mwanamke mpumbavu katika maisha yako, matokeo yake ni kama haya. Kumbe hata huyo mzee Abdul alijitahidi, kulea damu sio yako, eti alimpeleka mama hospitali kujifungua kumbe hata mtoto sio wake.

Matokeo ya kukutana na mtu asiye sahihi kwako.
 
Eli79 sasa kama Abdul alikua analala na mama nasib nyumbani kwa wazazi wake alipopata uchungu angebaki nyumbani na mamamkwe halafu majirani ndio wampeleke Amana!?

Mama Nasib kasema ni kweli alimpeleka hosp lakini hajawahi mlea nasib...... inaelekea mzee nae alikua analelewa tuu
 
Back
Top Bottom