Mwanaume usiye na kazi usipende!

Mwanaume usiye na kazi usipende!

Maswali kwa wadada na mtoa mada:

KWA MTOA MADA:
1)Vipi kama mwanaume umeajiriwa ila unalipwa 150k kwa mwezi hlf uko dar, au hata mkoani, una tofauti gani sana na jobless? Mifano hai ninayo, nina washkaj wameajiriwa ila hawawezi hata kuoa, sababu mshahara wao ni mdogo mno.

KWA WADADA:
2) Wadada mnataka wanaume wenye uchumi stable/wenye pesa za kutosha, ukifanya sensa ya kipato hapa Tanzania, ni asilimia ngapi ya vijana wa kiume walio kwenye umri wa kuoa (miaka 18-35) wanaopata walau tshs. Million 1 kwa mwezi? Na chances za wewe mdada kutongozwa na mkaka mwenye kipato cha hivo ni asilimia ngapi? Kelsea Dream Queen Demi Kalpana Dr criminal
Kutongozwa utatongozwa na wa aina mbali mbali, wenye nazo na wasio kuwa nao.

Pia anaweza akawa nazo na asiwe mtoaji. Ni kubahatosha tu
 
Kutongozwa utatongozwa na wa aina mbali mbali, wenye nazo na wasio kuwa nao.
Pia anaweza akawa nazo na aside mtoaji. Ni kubahatosha tu

Hata mkibahatika kupata wanaume wenye hela na ni watoaji, mara nyingi huwa mnawapiga na vitu vizito.

Kuna documentary moja niliona YouTube, mzungu mmoja mwenye pesa alimpenda binti wa kifilipino, binti alikuwa anapewa $1000 ya matumizi kila mwezi, ndugu za binti walijengewa ghorofa, binti alipangiwa nyumba kwenye best neighborhoods kule ufilipino na binti aliwekewa beki 3, binti alikuwa hafanyi kazi yoyote anaishi kwa raha.

Cha ajabu binti alitumia hiyo hela kumnunulia pikipiki Mkaka security guard, ambaye mshahara wake wa mwaka ndo hela anayopewa binti kwa mwezi, mkaka security guard na huyo binti walipanga njama wakamuua mzungu wa watu ili wao wabaki na mali waoane waishi pamoja, binti aligundulika akahukumiwa life sentence, cha ajabu siku ya hukumu hakuna hata ndugu wa binti mmoja aliyekuja mahakamani Demi
 
Jambo la msingi sana hili, nalo tukalituzame.

Lakini ukweli sasa hivi ukitaka kufurahia maisha tafuta kiasi chako, kubaliana na mtu, kutaneni sehemu muwekane hadi hamu zikate, mlipe ujira wake then tembea.

Haya mambo ya permanent relationship hata wenye ajira zao bado ni mtihani na mzigo mzito. Kulea wanawake nacho ni kipaji...
 
Pesa sio kila kitu ingawa ni muhimu iwepo.
Unaweza ukapewa pesa nyingi lakini nyege hazimalizwi, au mtu ana maudhi yasiyoisha.

Kitu mapenzi ni complicated, binadamu haturidhiki.
Ninachotaka kusema ni kuwa mwanaume unaweza ukawa na hela nyingi, tena ukawa husband material mwenye tabia njema, ila kama mwanamke hajavutiwa na wewe kimapenzi, hilo pia linaweza kuwa tatizo kubwa sana, kama huyo mwanamke hatokua mvumilivu mahusiano hayatodumu Demi
 
Usiwaondolee wenzio ujasiri wa kujiamini.

Inategemea.

Kuna wanawake wanakazi na hela na wanachotaka kwa Mwanaume ni penzi na heshima na uaminifu na sio pesa.

Si wanawake wote wapo after money.

Though kwa bongo ni wachache sana!
 
Mwanaume anaweza kuwa ni jobless leo lakini kesho akawa akapata kazi nzuri tu.

Ewe mwanamke mfurahie Mwanaume wako atazidi kukupenda hata akija kupata hela (ijapokuwa itategemea maana wengine nasikia hubadilika) akishapata hela hashikiki kwa umalaya.

Kama Mwanaume ametulia anakuheshimu basi usimdharau, usimchoke, usimfanyie visirani n..k.
 
Back
Top Bottom