Mwanaume wewe ni kichwa cha familia sio kila siri yako na madhaifu yako mkeo aijue

Mwanaume wewe ni kichwa cha familia sio kila siri yako na madhaifu yako mkeo aijue

Jemima Mrembo

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
2,864
Reaction score
8,328
Leo taasisi ya ndoa inapitia magumu mengi sana. Wababa hawajui wajibu wao na hawajui namna ya kuishi na mke kwa akili.

Mwanamke ametoka kwenye ubavu mmoja tu wa mwanaume, hivyo basi mwanaume unatakiwa uwe kichwa hasa.

Wanaume wengi wa leo wamelelewa na kina mama peke yao, hawajui kina baba wanatakiwa wafanyenini.

Usimwambie mkeo mapungufu na madhaifu ya mama yako na ndugu zako, ataudharau ukoo mzima. Mabinti wengi wa leo hawana upendo wa dhati, hawana hofu ya Mungu, hawana adabu, na wana dharau, jeuri na kiburi.
Pia wana matusi, masengenyo, na kila aina ya tabia mbaya.

Kama unafanya biashara si vyema mkeo ajue, hadi umejiridhisha. Mwanamke ndiye chanzo la anguko la mwanaume. Eva alimwangusha Adam. Delilah alimwangusha Samson.

Mwanaume tumia akili zako vizuri na usijaribu kutumia hisia kuongoza ndoa yako. Hisia tumeumbiwa wanawake, nyie mmeumbiwa akili.

Weekend njema
 
IMG_5295.jpg
 
Mambo ya u Beijing yanaharibu ndoa. To yeye mi sina cha kukuficha. Hata nikiwa na ndyeki ntakuambia. Hata kama nina ndusu utajua tu
Na usinifiche ila kama kuna kitu unadhani nikikijua kitakuletea udhaifu mbele yangu naomba nisikijue.....Mimi naweza chukulia poa lakini katika kutokuelewana kidogo wewe utajiwazia ananifanyia ivi Kwa sababu nilimwambia ivi
 
Back
Top Bottom