Mwanausalama Tanzania aaibika kutumia nguvu na mwanausalama wa Obama kumlinda mwandishi

Mwanausalama Tanzania aaibika kutumia nguvu na mwanausalama wa Obama kumlinda mwandishi

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925
Mwandishi wa Gazeti Uhuru anayejulikana kwa jina Selina Wilson alienda makumbusho ambako kulikuwa na ugeni mzito wa Mke wa Obama Michelle Obama kwa mwenyeji wake Salma Kikwete. Selina alikuwa na kitambulisho kilichoonyesha kuruhusiwa Symbion, lakini jina lake lilikuwepo kwenye orodha ya pale Makumbusho.

Kiongozi wa usalama Tanzania alimtilia nguvu mwandishi Selina Wilson na kumsukuma kwa nguvu atoke kwamba kitambulisho chake hakiruhusu kuingia pale ingawa jina lake lipo.

Mwanausalama wa Marekani aliingilia kati na kumwambia mwanausalama wa Tanzania kosa la kitambulisho si hoja ya kumfukuza kwa nguvu kwa sababu jina lake limo kati ya waandishi wa habari walioruhusiwa kuwepo pale.

Mwanausalama wa Marekani alienda mbali zaidi kwa kumwambia:
"Ndivyo mnavyofundishwa katika utendaji wenu"? Mwanausalama huyo wa Obama alikasirishwa sana na kitendo kile cha udhalilishaji kilichofanywa na mwanausalama wa Tanzania, akaamua mwandishi Selina Wilson aingie kufanya kazi yake kwa vile jina lake lipo.

Tukio hili ni la aibu sana kwa wanausalama wetu walivyo wanyanyasaji kwa wananchi na vyombo mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari nchini.


Chanzo: http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/13683-rais-oboma-atua-dar-na-familia-kwa-kishindo
 
... Wanafundishwa kutumia vitu veneye ncha kali na mijiguvu isiyo na weledi wowote ... Mwanausalama wa Tz mbona asitumie bomu kutoka china kumlipua mwanausalama wa USA? Si Kagonja ata m Cover???
 
Safi sana mkuu kwa taarifa ila hawa iron boys wa tanzania wanasafari ndefu na kikubwa kinachowaponza ni sifa na kutokutumia weledi akifikiri kutumia nguvu ataonekana anamlinda sana mke wa obama kumbe zoba
 
I am tired bwana! ngoja aondoke Obama mprempre wa kumbana pinda ndio habari ya town
 
Hiyo mipoliCCM,ishazoea kufanya madudu ya aina hiyo,si mnakumbuka namna Kamanda Kamuhanda,alivyoamrisha mauajiya mwandishi Mwangosi,ambapo hadi sasa huyo Kamuhanda hakupandishwa kizimbani kujibu tuhuma za mauaji,na badala yake,bosi wake JK,amempandisha cheo,kwa utumishi uliotukuka wa kumwua Mwangosi!

Kwa hiyo hata wale wanaofikiri ile kauli ya Pinda,ya kusema PIGA TU TENA WAPIGWE SANA KWA KUWA TUMECHOKA.

Hiyo siyo kauli ya Pinda as an individual,bali huo ndio msimamo wa serikali nzima ya CCM.

Kumbuka JK,alipotoa siri kwenye mkutano mkuu wa CCM,uliopita,alipowaasa wanaCCM wenzake,wapunguze kuwatumia poliCCM,kuwabeba kwenye shughuli zao za kisiasa!!
 
hakuwa na bomu tu vinginevyo ange Mwangosi au ange mchadema soweto arusha..

AH AH NIMEFURAHI SANA HATA MIPOLICCM ILIPIGWA MARUFUKU KUHUSIKA UWANJA WA NDEGE,

SAFI SANa FBI VERY BRIGHT KTK MASUALA YA USALAMA LKN POLICCM AKILI ZMELALA MASABULINI
 
Good News! Safi Sana! Hatimaye unyama wa serikali nje nje tu. Uovu wao unajianika wazi mbele ya watu wa dunia ya kwanza. Katika mafunzo yao ya kazi hakuna kitu 'taratibu'. Kwao kila kitu wao ni matumizi ya nguvu za ziada ni 'piga ua'. Wacha waumbuliwe na kufedhehesha mabosi wao akina 'Liwalo na liwe bin Piga ua tu'!
 
Mnyamwezi wa roho ujue hapo kaona avunje itifaki za kuingilia sehemu ya usalama ya nchi isiyo yake ili kutetea muandishi wa habari.

Halafu wanausalama wa bongo wameshindwa kumkatalia, kwanza mtu anatema yai tu watu wanajikanyaga kumjibu.

Umasikini tabu sana. Hasa wa mawazo.
 
Sasa huyo mwanausalama wa Bongo kwa nini alishindwa kumdunda huyo mwanausalama mwingine? SI AMEAMBIWA APIGE TU..?? Huyo mwanausalma wa Bongo akamatwe kwa kushindwa kutekeleza amri ya waziri mkuu, kwamba AMECHOKA WAPIGWE TU
 
Kwanza tujiulize Kidhungu chenyewe alikielewa? Ukute lilipoona linasemeshwa na Mdhungu likasogea pembeni kama halijasikia kitu! AIBU YAO, AIBU YA DHAIFU! Mapolice wetu wanaogopa Kidhungu ni mwisho. Siku 1 tunatoka Kigoma tunaelekea Kasulu dereva wangu akawa amechoshwa na tabia ya mapoliccm wanaosimama njia panda ya Mwandiga ya kulazimisha lift kwa watu wao. dereva akaniomba nisiongee nao Kiswahili. Nilipotema jamaa alirudi nyuma kwa kasi ya ajabu! Sasa na huyu Form 4 failure nina mashaka kama alikielewa, ndo maana hata mabishano hayakuwapo!
 
Ana bahati wangemrushia bomb,au kumng'oa kucha na meno bila ganzi unacheza na TISS wewe

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Aibu!, Aibu!, another thing an american was shocked was to see tht moron push and use such force on a WOMAN!
 
Ndivyo mnavyofundishwa katika utendaji wenu? Haya ni maneno mazito sana kuhusu maafisa wa usalama wetu.

Mkuu yaani hilo ni tusi zito sana.Duh!

"...NO NO Sir! We are not TEACHED that way. You know, you know we are AMRIzed to KICK if they NOT HEAR, we KICK ONLY, because us TIRED NOW..."
 
Huyo askari wetu alijibu nini baada ya kuulizwa kwa kimombo ikiwa hayo ndiyo wanayofundishwa katika utendaji wao?

Isije ikawa lugha ilikorofishwa akajibu yes Sir.
 
Back
Top Bottom