Mwandishi aliyeandika tuhuma za RC Simiyu adaiwa kukamatwa na Polisi
Duh...!, hizi mambo zimeanza tena?!..., au Maza nae anaelekea kuwa like Maza like Faza?!.
Tusubirie taarifa ya Edwin Soko wa MPC, kuthibitisha ni polisi maana Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama...
P
Pascal Mayalla awamu hii kila mtu anataka kula kwa urefu wa kamba yake. Yawezekana huyu mwandishi yuko kwenye kamba ya sakata hili.
i
Maulidi Ktenge alipost clip moja kupitia Wasafi Media akawa anasoma ujumbe aliotumiwa na Nawanda (na na Nawanda alitumiwa na mbaya wake) kwenye simu yake baada tu ya taarifa za mwandishi huyo kusambaa. Ujumbe unamtishia Nawanda kwamba atakoma na hapo ni mwanzo tu. Na kwamba alionywa kuacha kufuatilia mambo ya watu hakusikia.

Hii inaonesha Kuna kitu kimpeikwa juu ya sakata hili.

Inakuwaje mtu mzima afanye ngono halafu ibumbuluke?? Pascal Mayalla unanikwaza sana kwamba na wewe na unguli wako wote unategemea vijitaarifa vya mitandao uchawara hivi. Kwann usikwee pipa na kwenda kupiga kambi huko ukaja na taarifa isiyokuwa na mashaka??
 
Kuna mwamba alisema hapo rock city ndo kiwanja chake, na alishamchukua kwa 50k na badae akataka nyongeza ili atoe kule jamaa akamwambia sio mdau wa kule, hako kabint ni shida since 2019, kuna boda alikula mvua 30 kisa hako ka bint kumsingizia kukabaka, soma comment ya mayalla
kwa hiyo ana uzoefu wa kufanya mchezo huo? Basi nacho kahojiwe vema kujua historia yake katika mchezo huo huenda ni kashetani fulani hivi
 
Ngoja tusubirie ukweli maana sasa inaonekana mkorogo umeanza. Ila mi nasema hata kama wanamdhibiti mama kutokana na uwezo wake namsifu akipata hizi habari za kidhalimu kuhusu wateule wake anawatema hapohapo. Mnakumbuka yuke naimu waziri wa sheria aliyetuhumiwa kumdhalilisha yuke kijana babati mama alimtema hapohapo. Na haka kakora siju alikateua kwa ushauri wa nani kakatema hapohapo. Kwa hili heko mama.
Yeah. Kashfa zingine bhana zinaweza kupigwa danadana ila sio hii manake inamchafulia na kuifedhehesha mno Serikali yake. Yes, Mama yuko smart- anamuondolea kinga chap' halafu anamwacha ili wenye kazi zao wacheze nae kiduku:SansDefault:
 
Kuna taarifa za kukamatwa kwa Mwandishi wa Habari, Dinna Maningo ambae pia ni mmiliki wa Dima Online aliyechapisha kwa mara ya kwanza taarifa ya tuhuma za aliyekuwa RC Simiyu kulawiti, mwandishi huyu amekamatwa Tarime usiku wa kuamkia Juni 13, 2024.

Taarifa za awali zinadai kuwa mwandishi huyu kakamatwa Tarime mkoani Mara na Askari kutoka mkoa wa Mwanza na amesafirishwa kwenda Mwanza .

Matukio Daima Media inamtafuta RPC wa Mara na Mwanza kwa taarifa kamili.

CHANZO - MATUKIO DAIMA MEDIA

============

Awali, kulikuwa na taarifa kuwa amesafirishwa kwenda Mwanza lakini Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC), Edwin Soko amesema “Ni kweli tumejulishwa kuwa baada ya kukamatwa akiwa Tarime walitaka kumleta Mwanza na wakati wanaondoka naye wakasema wanamleta Mwanza ila huku hajafika, inavyoonekana yupo hukohuko Tarime.”

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC), Mugini Jacob amesema “Alikamatwa na Askari Polisi, jana jioni majira ya Saa Mbili Usiku (Juni13, 2024), akafikishwa Kituo cha Polisi Tarime, nilionana na Dinna lakini alikuwa hajaambiwa kosa lake ni lipi.”

JESHI LA POLISI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya, SACP Mark Njera hajapatikana kuzungumzia kinachoendelea.

=================

Mara Press Club yaliomba Jeshi la Polisi Mwanza kuweka wazi tuhuma za mwandishi wa habari Dinna

Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC) imeliomba Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kuweka wazi tuhuma zinazomkabili mwandishi wa habari wa blogu ya Dima Online, Dinna Maningo.

“Tuna imani Jeshi la Polisi mkoani Mwanza litatoa taarifa kuhusu tuhuma zinazomkabili mwandishi na mwanachama wetu wa Mara Regional Press Club, ndugu yetu Dinna Maningo bila kuchelewa," Mwenyekiti wa MRPC, Mugini Jacob amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Juni 14, 2024.

Jacob amesema Dinna alikamatwa nyumbani kwake mjini Tarime, Mara jana majira ya saa mbili usiku na hadi leo mchana alikuwa anashikiliwa katika kituo cha polisi Tarime

“Mara tu baada ya kukamatwa kwa Dinna nilipata taarifa na nilifika kituo cha polisi Tarime, tukaonana, alikuwa vizuri lakini aliniambia polisi waliomkamata hawakumwambia sababu ya kumkamata," Jacob amesema kwa kifupi.

Jacob amesema leo Ijumaa pia amefika katika kituo cha polisi Tarime na kuonana na Dinna ambapo amemueleza kuwa askari polisi waliomkamata wamemwambia wanamsafirisha kwenda jijini Mwanza wakati wowote kuanzia sasa.

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo amesema MRPC inawasiliana kwa karibu na uongozi wa Mwanza Press Club ili kusaidiana kufuatilia tukio hilo.

“Tuna imani jeshi letu la polisi litafanya kazi yake kwa weledi ili haki iweze kutendeka kwa wakati," amesema Jacob.

Chanzo: maraonlinenews
Huyu ni lazima akamatwe kwa sababu tuwezekano mkubwa ni kwamba ukio lhili lilikuwa ni dili; wanaweza kuwa wamepewa pesa hawa
Huyu ni halali kabisa kukamatwa
 
Huyu ni lazima akamatwe kwa sababu tuwezekano mkubwa ni kwamba ukio lhili lilikuwa ni dili; wanaweza kuwa wamepewa pesa hawa
Huyu ni halali kabisa kukamatwa
Deal wakati victim kaenda ku-report mwenyewe na ameenda kutoa vipimo kama ushahidi.

Mabaradhuli kama nyie mnaotetea huo ushenzi utakuta ndio tabia zenu kuwachukua mabinti kuwalewesha saa zingine kuwawekea mihadharati na kuwafanyia mambo ya hovyo.

Huyo mkuu wa mkoa kabaka hakuna kingine. Watu wanaotetea ujue na wenyewe ndio tabia zao.

Serikali inatakiwa kumfanya huyo mkuu wa mkoa mfano kama njia ya kuwapa nguvu na imani wanawake kujitokeza. Kwa sababu inaonekana kuna mijitu mingi inatabia hizo na yenyewe inaona matendo yao sawa.

Utakuta kuna wanawake wengi sana wapetia rape za namna hiyo wanaona aibu tu kujitoleza.

Useless kabisa watu kama nyie, ningekuwa mod natoa tu ID zenu kwa ndugu na jamaa waje walipe visasi kwenu.
 
Deal wakati victim kaenda kaenda ku-report mwenyewe na ameenda kutoa vipimo.

Mabaradhuli kama nyie mnaotetea huo ushenzi utakuta ndio tabia zenu kuwachukua mabinti kuwalewesha saa zingine kuwawekea mihadharati na kuwafanyia mambo ya hovyo.

Huyo mkuu wa mkoa kabaka hakuna kingine.
Hakuna kitu kama hicho broo. Walikuwa na mahusiano ya muda mrefu halafu hao ni watu wazima(Adults). Huyo binti ni mzoefu ila sema tu Dili (tozo)lilibumba
na kwa uzoefu wake akajua la kumfanya huyo kidume ili kumkomoa. Na kweli kamkomoa.
 
Mimi wala sina tatizo tundu gani kaingiliwa na kwa umri wake sheria inamruhusu kufanya tendo la ndoa na mtu wa umri wa rika linaloruhusiwa.

Shida ni kwamba hata kama huyo dada angekuwa mtu wake wa kila siku au malaya anaeijiuza na washakutana mara kadhaa.

Iła siku inayolalamikiwa huyo dada akutaka kutoa mzigo sasa it doesn’t matter ni mtu wake au la; kumuingilia mtu bila ya idhini yake ni ubakaji simple as that.

Halafu kiongozi gani ana tabia za hovyo kuparamia watu kwenye magari nje ya bar hilo tu tosha kufukuzwa kazi hata kama ingekuwa consensual act.

Jamaa ni mtu wa hovyo na serikali imepata ‘scapegoat’ ya kutuma salamu kwa wengine. Kama wanaweza deal na kigogo basi wengine wajue hawako salama na hizo tabia jeshi la polisi aiwezi vumilia ni ubakaji wa kutumia kilevi.

Hii kesi kama wako serious na hali mbaya ya mmomonyoko wa maadili inayoendelea huyo mkuu wa mkoa anatakiwa kuwa mfano wa kutuma salamu kwa wengine kwenye jamii.
 
Kuna taarifa za kukamatwa kwa Mwandishi wa Habari, Dinna Maningo ambae pia ni mmiliki wa Dima Online aliyechapisha kwa mara ya kwanza taarifa ya tuhuma za aliyekuwa RC Simiyu kulawiti, mwandishi huyu amekamatwa Tarime usiku wa kuamkia Juni 13, 2024.

Taarifa za awali zinadai kuwa mwandishi huyu kakamatwa Tarime mkoani Mara na Askari kutoka mkoa wa Mwanza na amesafirishwa kwenda Mwanza .

Matukio Daima Media inamtafuta RPC wa Mara na Mwanza kwa taarifa kamili.

CHANZO - MATUKIO DAIMA MEDIA

============

Awali, kulikuwa na taarifa kuwa amesafirishwa kwenda Mwanza lakini Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC), Edwin Soko amesema “Ni kweli tumejulishwa kuwa baada ya kukamatwa akiwa Tarime walitaka kumleta Mwanza na wakati wanaondoka naye wakasema wanamleta Mwanza ila huku hajafika, inavyoonekana yupo hukohuko Tarime.”

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC), Mugini Jacob amesema “Alikamatwa na Askari Polisi, jana jioni majira ya Saa Mbili Usiku (Juni13, 2024), akafikishwa Kituo cha Polisi Tarime, nilionana na Dinna lakini alikuwa hajaambiwa kosa lake ni lipi.”

JESHI LA POLISI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya, SACP Mark Njera hajapatikana kuzungumzia kinachoendelea.

=================

Mara Press Club yaliomba Jeshi la Polisi Mwanza kuweka wazi tuhuma za mwandishi wa habari Dinna

Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC) imeliomba Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kuweka wazi tuhuma zinazomkabili mwandishi wa habari wa blogu ya Dima Online, Dinna Maningo.

“Tuna imani Jeshi la Polisi mkoani Mwanza litatoa taarifa kuhusu tuhuma zinazomkabili mwandishi na mwanachama wetu wa Mara Regional Press Club, ndugu yetu Dinna Maningo bila kuchelewa," Mwenyekiti wa MRPC, Mugini Jacob amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Juni 14, 2024.

Jacob amesema Dinna alikamatwa nyumbani kwake mjini Tarime, Mara jana majira ya saa mbili usiku na hadi leo mchana alikuwa anashikiliwa katika kituo cha polisi Tarime

“Mara tu baada ya kukamatwa kwa Dinna nilipata taarifa na nilifika kituo cha polisi Tarime, tukaonana, alikuwa vizuri lakini aliniambia polisi waliomkamata hawakumwambia sababu ya kumkamata," Jacob amesema kwa kifupi.

Jacob amesema leo Ijumaa pia amefika katika kituo cha polisi Tarime na kuonana na Dinna ambapo amemueleza kuwa askari polisi waliomkamata wamemwambia wanamsafirisha kwenda jijini Mwanza wakati wowote kuanzia sasa.

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo amesema MRPC inawasiliana kwa karibu na uongozi wa Mwanza Press Club ili kusaidiana kufuatilia tukio hilo.

“Tuna imani jeshi letu la polisi litafanya kazi yake kwa weledi ili haki iweze kutendeka kwa wakati," amesema Jacob.

Chanzo: maraonlinenews
Matukio haya sasa yamezidi sio chini ya mara5 naskia hz mambo sasa hzo haki zi nazosifiwa kila siku haki za waandishi zko wapi? Au ndo danganya totoo!!
 
Nchi ngumu sana hii. Hapo atatafutiwa kesi ya utakatishaji fedha, uchochezi, ukiukaji wa maudhui ya kuweka taarifa mtandaoni, kuendesha chombo cha habari huku akiwa hana kibali, nk.
Why the negativity? Kwa nini usiheshimu kazi za wenziyo ukasubiri taarifa rasmi? Activists!
 
Back
Top Bottom