Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Una uhakika hao unaotaka niwaheshimu wanafanya kazi zao kwa umakini na weledi?Why the negativity? Kwa nini usiheshimu kazi za wenziyo ukasubiri taarifa rasmi? Activists!
Kingine alikuwa na kesi za kuibia wadau simu na hela, kwa hiyo alikuwa anatafutwa.Huyo hakuwa na back up tu, angepata wazoefu wakampa shule angekusumbua sana tu
Shida ni kutumika na kuahidiwa 10000 shida ipo hapaDuh...!, hizi mambo zimeanza tena?!..., au Maza nae anaelekea kuwa like Maza like Faza?!.
Tusubirie taarifa ya Edwin Soko wa MPC, kuthibitisha ni polisi maana Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama...
P
Hakuna cha kurefusha mchakato ni very simple.Kujulikana unajulikana vizuri ila isingekua kirahis kama alivodakwa saiv...wangerefusha mchakato!
Urahisi wake ni upi?Hakuna cha kurefusha mchakato ni very simple.
unaambiwa ni katoa tigo kalikokubuhu, inawezekana mh hakukafukunyua vzuri ndo maana kakaleta za kuleta, hako katoto ni kashetan, some comment ya mayala utaelewa ushetwain wa [/QUOTE]unaambiwa ni katoa tigo kalikokubuhu, inawezekana mh hakukafukunyua vzuri ndo maana kakaleta za kuleta, hako katoto ni kashetan, some comment ya mayala utaelewa ushetwain wa hako katoto.kwa hiyo ana uzoefu wa kufanya mchezo huo? Basi nacho kahojiwe vema kujua historia yake katika mchezo huo huenda ni kashetani fulani hivi
Umesema ukweli kabisa!Uwezo wa huyu mama kuongoza nchi ni mdogo mno,anapenda kusifiwa tu kama alivyokuwa Magufuli,kuna makumi ya watu wamepotea Tangu Samia awe Rais,bado Tanzania siyo salama hata kidogo kwa waandishi werevu wa Habari,labda makanjanja ya CCM ndo yapo salama,yote kwa yote, MUNGU yupo,yuko wapi Magufuli?
Duniani tunapitia ttu,acha watese watu ipo siku yao.
Tunaombeni picha yake basi tuione. Kumbuka kesho ni siku ya Mabaharia Duniani.hako kabint hata ukiangalia picha yake kwa jicho la 3 utagundua tu kuwa hakafai, sema sura na shape inawaweka wana mtegoni.
Kama ameitwa kwa heri na si shari kama unavyodai, ilishindikana nini kumpigia simu ya wito na akaenda mwenyewe Polisi station badala ya hiki walichokifanya Polisi?Hapa Mkuu umenena vyema.Huyu ndiye aliyefichua mambo.Kuna ubaya gani kwenda kutoa ushirikiano polisi ? Tatizo watu wana midomo mirefu kama chupa,Kazi umbea tuuuuuu,
Hili la ufiraji na ubakaji walitaka kuliweka chini ya kapeti, lakini limewazidi kimo.Nchi mama imemshinda, inaonekana kuna serikali nyingi tu kila mahali
We zingua uone ilivyo simpo, siwezi toa siri za kambi mkuu ila ogopa sana hizi devices.Urahisi wake ni upi?
Kuna taarifa za kukamatwa kwa Mwandishi wa Habari, Dinna Maningo ambae pia ni mmiliki wa Dima Online aliyechapisha kwa mara ya kwanza taarifa ya tuhuma za aliyekuwa RC Simiyu kulawiti, mwandishi huyu amekamatwa Tarime usiku wa kuamkia Juni 13, 2024.
Taarifa za awali zinadai kuwa mwandishi huyu kakamatwa Tarime mkoani Mara na Askari kutoka mkoa wa Mwanza na amesafirishwa kwenda Mwanza .
Matukio Daima Media inamtafuta RPC wa Mara na Mwanza kwa taarifa kamili.
CHANZO - MATUKIO DAIMA MEDIA
============
Awali, kulikuwa na taarifa kuwa amesafirishwa kwenda Mwanza lakini Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC), Edwin Soko amesema “Ni kweli tumejulishwa kuwa baada ya kukamatwa akiwa Tarime walitaka kumleta Mwanza na wakati wanaondoka naye wakasema wanamleta Mwanza ila huku hajafika, inavyoonekana yupo hukohuko Tarime.”
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC), Mugini Jacob amesema “Alikamatwa na Askari Polisi, jana jioni majira ya Saa Mbili Usiku (Juni13, 2024), akafikishwa Kituo cha Polisi Tarime, nilionana na Dinna lakini alikuwa hajaambiwa kosa lake ni lipi.”
JESHI LA POLISI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya, SACP Mark Njera hajapatikana kuzungumzia kinachoendelea.
=================
Mara Press Club yaliomba Jeshi la Polisi Mwanza kuweka wazi tuhuma za mwandishi wa habari Dinna
Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC) imeliomba Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kuweka wazi tuhuma zinazomkabili mwandishi wa habari wa blogu ya Dima Online, Dinna Maningo.
“Tuna imani Jeshi la Polisi mkoani Mwanza litatoa taarifa kuhusu tuhuma zinazomkabili mwandishi na mwanachama wetu wa Mara Regional Press Club, ndugu yetu Dinna Maningo bila kuchelewa," Mwenyekiti wa MRPC, Mugini Jacob amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Juni 14, 2024.
Jacob amesema Dinna alikamatwa nyumbani kwake mjini Tarime, Mara jana majira ya saa mbili usiku na hadi leo mchana alikuwa anashikiliwa katika kituo cha polisi Tarime
“Mara tu baada ya kukamatwa kwa Dinna nilipata taarifa na nilifika kituo cha polisi Tarime, tukaonana, alikuwa vizuri lakini aliniambia polisi waliomkamata hawakumwambia sababu ya kumkamata," Jacob amesema kwa kifupi.
Jacob amesema leo Ijumaa pia amefika katika kituo cha polisi Tarime na kuonana na Dinna ambapo amemueleza kuwa askari polisi waliomkamata wamemwambia wanamsafirisha kwenda jijini Mwanza wakati wowote kuanzia sasa.
Hata hivyo, Mwenyekiti huyo amesema MRPC inawasiliana kwa karibu na uongozi wa Mwanza Press Club ili kusaidiana kufuatilia tukio hilo.
“Tuna imani jeshi letu la polisi litafanya kazi yake kwa weledi ili haki iweze kutendeka kwa wakati," amesema Jacob.
Chanzo: maraonlinenews
==================
=====
Pia soma: MCL: Mkuu wa Mkoa adaiwa kumlawiti mwanafunzi wa SAUT