'MTEKAJI' WANAHABARI WA SAFARI HII NI KAMANDA MBOWE NA TAYARI MWIGULU NCHEMBA ANALO TOLEO JIPYA LA SINEMA HIYO YA 'COMING SOON IN TOWN'
Mwigulu Nchemba hebu rudi haraka kutoka huko JKT ukatuchongee mkanda mwingine maana kwa sasa yule mtaalam mwenzako, Joseph Ludovick, hapatikani tena mtaani.
Kwenye huo mkanda mpya napendekeza Kamanda wetu wa Anga, Freeman Mbowe, ndiye awe mhusika mkuu kwa kuwa uhusika mkuu wa Kamanda Lwakatare wala haikunoga saaana vile.
Hebu katumie ile ile Teknolojia ya Kikatuni (Animation) ili ukamlishe Kamanda Mbowe anavyopanga kumteka mfanyakazi wake mwanahabari wa pale pale Tanzania Daima kwa kuwa wameonekana kumuandika vibaya sana pamoja na chama chake CHADEMA.