Mwandishi Andrew Chale anusurika kutekwa na watu wasiojulikana

Mwandishi Andrew Chale anusurika kutekwa na watu wasiojulikana

Kama watekaji ni polisi utaenda kuripoti polisi kwa lengo gani? Maana hata kama walikuwa hawana uhakika na sura yako na mahali unapoishi, ukienda kuripoti ndiyo utakuwa umewarahishia.
Eeh! ameripoti kituo kipi cha Usalama?
 
Makubwa hivi baba wa nyumba Hii yupo hai kweli?
 
CDM wanataka kutengeneza move mpya ili tusahau ya Gaidi Lwakatare na Mtandao wake wa kigaidi wa chadema. Huyo mwandishi wa Free Media chini ya Mbowe amepewa maelekezo aigize.Hapa hapotezwi mtu. Huko analogia tulishahama tuko Digital kajipangeni upya.

mmmh! Harufu mbaya hii, hv wewe unawaza kwa kutumia makalio? We unadhani kati ya waliomkamata lwakatare na lwakatare mwenyewe nani gaidi? Pumbavu!
 
Waandishi wa habari wameundiwa hali ya kuamini kuwa mbaya wao ni Lwakatare na kwa vile sasa yuko ndani basi wako salama,
Kalagabao

acha ujinga we KAMAKABUZI, kwn huyo lwakatare ameshathbitishwa na mahakama kuwa anahatia? Acha ku2mia makalio kufikiri.
 
WanaJF tutasikia matukio haya na kuona mambo mangapi ili watanzania tuamke usingizini?? Naona kuna jambo la ziada la kufanya.
 
acha propaganda.

Dar es Salaam

MWANDISHI wa Habari wa Gazeti la Tanzania Daima Andrew Chale ameanza kuishi maisha ya wasiwasi baada ya watu wasiojulikana kufanya jaribio la kumteka.

Chale alisema kwamba siku ya Jumamosi usiku watu wasiojulikana walikuwa wakifuatilia nyedo zake.

Alisema watu walikuwa kwenye magari mawili yenye rangi na namba za Jeshi la Polisi walikuwa wakimfuta nyuma kila alipokuwa akipita kuelekea nyumbani kwake maeneo ya Sinza jijini Dar es Salaam.

"Siku ya Jumamosi usiku nikiwa njiai kutoka Kazini, niliona magari mawili ya Polisi yakinifuata kwa karibu na baada ya kuingia uchochoro flani wakuingia nyumbani magari hayo yakapaki"alisema Chale na kuongeza"
"Watu waliokuwa eneo hilo walisema kwamba baada ya magari hayo kupaki wakakaa hapo kwa saa mbili na baadaye walishuka askari watu huku wawili wakivaa nguo za kiraia huku mmoja akiwa na Gazeti la Tanzania Daima mkononi".

Alisema kwamba baada ya watu hao kushuka na kuuliza mtu waliemwita kwa jina la ANDRESON,, ndipo wakaambiwa kwamba hakuna mtu mwenye jina hilo katika mtaa huo lakini , walipoelezea mwonekano wake, wakajibiwa kuwa kijana anayefahamika eneo hilo hupita tu lakini mahali anapoishi hapajulikani.

"Tunayemfahamu ni kijana mmoja ila huwa anapita hapa akiwa na hilo Gazeti majira ya usiku, na wakati mwingine huwa anapita hapa akiwa na mambo yake mengine, baaada ya hapo magari hayo yaliondoka"aliwanukuu mashuhuda wa tukio hilo.

"Watu hao walirudi tena hadi nyuma ya nyumba yangu na nikawasikia wakijitambulisha kuwa wao ni Polisi jamiii na kwamba walikuwa wakimtafuta kijana mmoja ambaye wamesahau anapoishi"alifafanua Chale.



source habarimpya.com
 
Back
Top Bottom