Mwandishi Andrew Chale anusurika kutekwa na watu wasiojulikana

Waandishi hawajaipa uzito habari ya kutekwa kibanda badala yake wanaona mtekaji lwaka ameonewa

Hakuna post ambayo nitaitembelea nikose shudu lako lolote hongera sanaaaaaa..... sijui unafanya kazi saa ngapi na unahudumia kwel mkeo vizuri...... @ utaifakwanza mmmh! mpaka 2015 tutasikia mengi sanaaaaaaa
 
Mungu anusuru hilo balaa, waandishi muache kushabikia wauwaji muwe neutral.muige kenya
Utaifakwanza...hivi utaifa utakuwepo ikiwa watu wanaounda taifa wanauwawa...na kuumizwa kwa 'makusudi'!?

Kwa kiasi fulani inaonyesha dhahiri una kerwa na msimamo wa waandishi...na maoni/ushauri wako kwao ni kama unawatukana...yaani unataka kuuaminisha umma kuwa waandishi hawana uwezo wa kutambua na kutafakari haya yanayotokea juu ya wenzao!?

Nikipata muda nijaribu kutafuta ukweli kama unamfahamu 'NNAPPE' wa ukweli.
 
Waandishi sasa badilisheni mbinu zamedani kama JF. kuweni invisible, no real names.
 
Hata kama wengine mnabwabwaja tu humu ndani kuwa Tanzania hakuna waandishi wa habari, lakini wengi wetu hata humu ndani tunatumia ID ambazo hazifahamiki (tunajificha) hao tunao wadharau kwangui naona wanajitahidi pamoja na mapungufu yao. Tusilaumu saana kama vile sisi tuko sahihi kihivo.
 
CDM wanataka kutengeneza move mpya ili tusahau ya Gaidi Lwakatare na Mtandao wake wa kigaidi wa chadema. Huyo mwandishi wa Free Media chini ya Mbowe amepewa maelekezo aigize.Hapa hapotezwi mtu. Huko analogia tulishahama tuko Digital kajipangeni upya.
 
Usaliti wa waandishi, Magogoni watawatisha mpaka mfanye walitakalo
 
Ndani ya hizo gari kulikua na Koleo la kung'olea kucha na meno,
Bisibisi ya kutobolea macho,
Marungu na nyundo,
Ila hakukua na Ganzi! !!!!
 
Hakuna namba ya gari.Watu wengine tunaweza kusema habari hii imepikwa ili kupoteza mwelekeo wa kufuatilia kesi ya msingi ya bwana Lwakatare.Kama umeliona gari la polisi, weka namba ya gari hapa, naamini uliiona plate number inayoanzia na "PT.....".malizia na namba zingine.kama hiyo gari ilisimama for dam 2 hours, ni hakika kwamba number yake inajulikana.na kwanini watembee na gazeti la Tanzania Daima, tena usiku?hao waliolisoma hilo gazeti, walilimulika na tochi?au waliwamulika hao polisi?au hapa kwetu hatuna "investigative journalism", tunaandika tu kuwatia hofu watu wengine.Kwa hiyo hata mwandishi akiwa barabarani akaona gari ya polisi ikiwa kwenye doria za kawaida anahisi anafuatiliwa?
 
baba amegonga mtu na kuendelea na safari akiwa na msafara wa magari mengi akifika atakuja na majibu nitamwambia

Inasikitisha sana yule mama namfahamu anakaa maeneo ya Bunju Shule nishawahi kukaa naye seat moja wakati naenda Bagamoyo akashukia kituo cha Bunju Shule.
 
Ukitaka amani, kawe mwandishi wa uhuru na daily news! au hamia tbc
 
tatizo la tanzania polis ni sehemu ya watuhumiwa kwenye matukio ya utekaji!
 
Waandishi wa habari wameundiwa hali ya kuamini kuwa mbaya wao ni Lwakatare na kwa vile sasa yuko ndani basi wako salama,
Kalagabao
 
Huu upumbavu wa nchi hii, halafu kova ndo atakuwa msemaji mkuu wa hilo, hawa polisi ndo watuhumiwa inakuwaje wao ndo wasemaji tene, jamani taifa linaangamia
 
Eeh! ameripoti kituo kipi cha Usalama?

nadhani hukuielewa habari. Wanaotaka kumteka ni wana usalama, kisha aende kujisalimisha au? Unamfundisha kesi ya nyani aipeleke kwa ngedere au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…