Mwandishi Ansbert Ngurumo apewa hifadhi kwa usalama wake nchini Finland

Mwandishi Ansbert Ngurumo apewa hifadhi kwa usalama wake nchini Finland

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Ni habari mbaya kwa nchi yetu inaendelea kuwa na hadhi mbaya ndani /nje ya mipaka yake. Maisha ya waandishi wa habari, wanasiasa na wanaharakati yamekuwa ya mashaka.

Mwanahabari Ansbert Ngurumo aliyewahi kuwa mhariri wa Magazeti ya Tanzania Daima na Mwanahalisi, amekimbilia nchini Finland na kupewa hifadhi huko, kwa muda alikuwa akisema anatishiwa kuuawa.

Habari zaidi soma=> Ansbert Ngurumo: Muda wowote naweza kufa maana natishiwa kifo

UPDATE:

Mwandishi wa Habari mwandamizi nchini, Ansbert Ngurumo amepata hadhi ya kupewa ulinzi nchini Finland, baada ya kudai amekimbia aliowaita "wauaji" wake.

Ngurumo ambaye amewahi kuwa mhariri wa magazeti kadhaa nchini; Mtanzania, Tanzania Daima na MwanaHalisi, ameiambia JamiiForums kuwa amekiepuka kifo kilichopangwa na wale aliowaita "wasiojulikana."

Akizungumza na JamiiForums, Ngurumo alisema ni kweli amekimbia Tanzania ili kuulinda uhai wake baada ya kuanza kuwindwa na watu wasiojulikana.

"Tangu mwaka jana nimekuwa nikipokea vitisho vingi na vyenye kuogofya kufuatia makala zangu kwenye gazeti la MwanaHalisi. Nimenusurika kuuawa mara kadhaa, lakini nashukuru Mungu hadi leo niko hai," anasema Ngurumo.

Anasema ili kunusuru uhai wake, alilazimika kujificha Mwanza tangu mwaka jana na baadaye kupata kwenda Kenya, kabla ya kwenda Sweden na sasa Finland, ambako amepewa hifadhi.

Ngurumo anasema hadhi aliyopewa Finland, siyo ya ukimbizini, bali ni "hifadhi ya kimataifa," kuunusuru uhai wa mtu ambaye yuko katika hatari ya kuuawa nchini mwake.

Vyombo vya Habari vya Finland na mitandao ya kijamii, imeandika habari ya Ngurumo kukimbia Tanzania kwa hofu ya kuuawa.

"Nimezungumzia mkasa wangu wa kunusurika kudakwa na watu wasiojulikana, ambao wamekuwa wakipanga kuniua na wamejaribu mara kadhaa bila mafanikio, sasa nikaona niwakimbie, kwani kufa kijinga ni dhambi kubwa," anaongeza Ngurumo.

JamiiForums inatambua kuwa Ngurumo alianza kuhofia maisha yake baada ya kudai kupokea vitisho kwa alichodai ni kufuatia kuandika makala kwenye gazeti la MwanaHalisi ikiwa na kichwa cha habari; “Tumuombee Rais Magufuli au Tundu Lissu?”
 
Hii ndio hali halisi, mambo mengi na mazito yataibuliwa huyu jamaa ikija kutoka madarakani. Ndivyo ilivyo hata wakati wa Hitler dunia ilikua haiamini story za ukatili uliokua unafanywa na serkali yake kilikua ni kitu ambacho hakiingii akilini.
Pengine huyu "kiongozi wa malaika" atakuja kulindwa na mrithi wake, ila ole wenu mnaotumika kutekeleza huo ukatili mtalipia matendo yenu kikamilifu.
 
Cha ajabu nini? Hata wewe ukitaka omba asylum popote kama sababu zako zitakuwa na mashiko watakupa, don't worry brother!
 
Ni habari mbaya kwa nchi yetu inaendelea kuwa na hadhi mbaya Ndani /Nje ya mipaka yake. Maisha ya waandishi wa habari, Wanasiasa na Wanaharakati yamekuwa ya mashaka.

Mwandishi Ansbert Ngurumo amepewa Asylum Nchini Finland sasa ni mkimbizi, kwa muda alikuwa akisema anatishiwa kuuwawa

Habari zaidi soma=>Ansbert Ngurumo: Muda wowote naweza kufa maana natishiwa kifo
Nashauri Lisu asuridi Tanzania, hawa wauaji watammaliza. Atutetee akiwa huko , it will also give big impact!
 
Back
Top Bottom