Miaka ya tisini kuna mshkaji alirudishwa kutoka Sweden.Ni miongoni mwa watu waliozamia kuondoka Tanzania kwa gia ya ukimbizi Zanzibar.
Alivyorudi akawa kaja maskani. Kuna mtu akawa anamsifia Nyerere. Jamaa akamponda sana Nyerere.
Akasema Nyerere ni sababu yeye karudishwa Tanzania.
Mshkaji anasema alipokuwa Sweden alikuwa anapeta kama mkimbizi, siku moja Nyerere akatembelea Sweden katika kazi zake za kimataifa baada ya urais. Watu wakamuuliza, Mwalimu Nyerere Tanzania inaelekea wapi siku hizi, mnatoahata wakimbizi wa kisiasa wanakuja kuomba hifadhi huku? Kulikoni?
Nyerere akasema wako wapi wakimbizi hao? Natakakuongea nao.
Akaambiwa tulia, tutakupeleka.
Akapelekwa mpaka kwenye mkutano na hao wakimbizi.
Nyerere akaanza kuwaluliza mmoja mmoja, wewe umetoka wapi. Kila mmoja anataja alipotoka.Ingawa walijikokikama Wazanzibari, wengi walikuwa watoto wa Dar.
Ilipofika zamuya mshkaji akaulizwa, akasema anatoka Faya. Nyerere akamhamakia "Faya hapa Mwembetogwa hapa? Kuna vurugu gani ya kukufanya uwe mkimbizi?". Nyerere alitumia jina la zamani la Faya "Mwembetogwa", kuonesha kwamba anapajua hapo kipindi kirefu tangu anaishi Magomeni.
Basi akawaambia wale wa Swidi, hapa hamna mkimbizi wa kisiasa,hawa vijana wote wanatafuta maisha wametoka Dar es salaam ambapo hakuna matatizo.
Siku chache baada ya hapo wakapandishwa ndege wakatupwa Bongo.
Jamaa tangu sikuhiyo hataki kumsikia Nyerere.
Nasikiyika kwa nchi yetu ilipo leo, watu wanaweza kujenga case credible ya kutafuta na kupata ukimbizi.