Mwandishi wa Habari mkongwe Gordon Kalulunga anadai kusakwa na Jeshi la Polisi kila Kona ya jiji la Mbeya.
Kwa maelezo yake Kalulunga anasema tarehe 6 mwezi huu saa sita mchana alipigiwa simu na Msaidizi wa OCCID wilaya ya kipolisi Mbalizi Christopher Makawia na kumwambia, "tukutane pale Benki ya NMB Mwakapangala jijini Mbeya kwa mazungumzo".
Kalulunga anadai alipofika alikuta gari la Polisi na maaskari wenye silaha za moto akapitiliza kuwapotezea.
Anadai, "aliendelea kunipigia lakini sikupokea kwa nini aniite maeneo yale na si kituoni".
Kalulunga anayemiliki blogu maarufu Mbeya ya Sauti ya Nyikani amekuwa mkosoaji wa matumizi ya Fedha za umma zinazoletwa mkoani humo.
"Nimepata taarifa kuwa ni DED ameagiza nikamatwe kueleza wapi ninatoa Siri za Serikali na kuandika mtandaoni".
Kalulunga ametoweka nyumbani kwake na ameeleza anaishi mafichoni kuhofia mazingira hayo.
My take: Haya mambo ya Polisi au Watumishi kutishia au kujenga uadui na wanahabari yaliachwa na kuondoka na awamu ya 5.