Mwandishi wa Habari Luqman Maloto afungua kesi dhidi ya DCI na DPP kisa Tundu Lissu, Azory Gwanda na Ben Saanane

Mwandishi wa Habari Luqman Maloto afungua kesi dhidi ya DCI na DPP kisa Tundu Lissu, Azory Gwanda na Ben Saanane

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mwanahabari Luqman Maloto, amefungua kesi ya jinai No. 5/2023 dhidi ya DCI na DPP Mahakama Kuu, Dar es Salaam, akiiomba itamke ofisi hizo zimeshindwa kuchunguza matukio yaliyofanywa na wasiojulikana ikiwemo kushambuliwa Tundu Lissu, kupotea Azory Gwanda na Ben Saanane.

Maloto.jpg

Maloto 1.jpg

Chanzo: MwanaHalisi

======

HABARI ZAIDI..

Matukio ya kupotea, kushambuliwa, kuteswa na kuuawa kwa baadhi ya watu wakiwemo wanahabari, wanasiasa na wasanii, sasa yamekabidhiwa mahakamani baada ya mamlaka zenye dhamana ya upelelezi kushindwa kutoa taarifa za upelelezi wa matukio hayo.

Matukio hayo yamefikishwa mahakamani na mwanahabari na mwanaharakati wa haki za binadamu, Luqman Maloto aliyefungua shauri la maombi ya jinai Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).

Katika shauri hilo namba 5 la mwaka 2023, Maloto pamoja na mambo mengine anaiomba mahakama hiyo itamke DCI anawajibika kwa maisha ya watu aliowataja ambao wamo waliopotea, walioshambuliwa na kuteswa na waliouawa kwa kuwa wajibu wake ni kulinda maisha ya Watanzania.

Maloto amewataja waathirika hao ni pamoja mwanahabari Azory Gwanda na wanasiasa Ben Saanane, Simon Kanguye, Daniel John, Tundu Lissu, Mdude Mpaluka Nyagali maarufu kama Mdude, Leopord Lwajabe, Akwilina Akwilini, Ibrahim Mshana maarufu kama Roma Mkatoliki na Allan Kiluvya.

Pia anaiomba mahakama hiyo itamke DCI ameshindwa ama kwa kutokuwa na uwezo au kwa makusudi kufanya upelelezi kuhusu madhila yaliyowakuta watu hao kutokana na kushindwa kutoa taarifa kwa umma na kwa familia za waathirika hao kuhusu madhila yaliyowapata.

Hivyo anaiomba mahakama hiyo itamke kwamba kuchelewa au kushindwa kukamilishwa kwa upelelezi dhidi yao hakuongozwi na kanuni yoyote na itoe amri dhidi ya DCI kuwasilisha mahakamani hapo taarifa yenye maelezo ya kina kuhusu kupotea, kuuawa na kuteswa kwao, kwa uchunguzi zaidi. Shauri limepangwa kusikilizwa na Jaji John Nkwabi na litatajwa Februari 8 mwaka huu.

Chanzo: Mwananchi

PIA, SOMA:
- Mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), Azory Gwanda apotea siku 10 na hajulikani alipo
 
Lakini hao wapumbavu huko walipo sirini wanateseka sana kumwaga damu isiyo hatia.
Ningekuwa ndugu ningewalipizia kisasi kuwapukutisha chain yote.
Namtafuta mtu mwenye phd ya uchawi anyoke nao kupitia maagano.
Ndo maana ya chain ni lazima upukutike likupate sababu si ulishiriki hatia. Kombora linapenya kwenye hatia.
 
Back
Top Bottom