TANZIA Mwandishi wa habari wa TBC Joachim Kapembe amefariki dunia

TANZIA Mwandishi wa habari wa TBC Joachim Kapembe amefariki dunia

Mocumentary

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
806
Reaction score
2,049
D051C076-5E1C-434A-8804-71449CEDE165.jpeg


Mwandishi wa habari wa TBC mkoani Manyara, Joachim Kapembe amefariki dunia Desemba 13, 2022 akishuka kutoka katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Kapembe aliungana na Waziri Nape Nnauye na viongozi wengine katika uzinduzi wa huduma ya intaneti kwenye kilele cha mlima huo.

Swahilitimes.
 
Mwandishi wa Habari na Mpiga picha wa Shirika la Utangazaji Tanzania Mkoani Manyara, Joachim Kapembe, amefariki dunia alipokuwa akishuka kutoka katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Marehemu pamoja na Watendaji wengine wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari walipanda Mlima huo mnamo Desemba 9, 2022.

Chanzo: EastAfrica Radio
 
Apumzike kwa aman..
Japo alikua yuko kazini Ila watu wasiwe wanaforce kupanda huo mlima bila kua na mazoezi ya kutosha, au unakuta mtu ana pressure na magonjwa yasiyoambukiza anataka nae akapande..
RIP, poleni mno kwa wafiwa na staff mates wake wote, mkuu ni haki yako kuchangia ila mimi hii issue nimeiona kwa upande wa pili, tumeshuhudia watu walio fit kabisa,gym kila siku na wana drop dead ndani ya gym, pia hapa kuna tatizo kubwa mno,uokoaji wetu pale mlimani bado ni wa kijima, nchi ilipata aibu mno kipindi kile yule celebrate kutoka SA alipofia mlimani wakati uzuzu ule unafanyika wa kumkimbiza chini kwa kutumia mkokoteni, Ile ni aibu na kama nchi hatujifunzi, juzi kati tumeionyesha dunia jinsi ya kuokoa ndege kwa kamba na mitimbwi!
 
Yale Yale ya wapo busy kukopa ,wapo busy tozoooooo,kuweka mazingira ya uokoaji ni 00000000 delete ccm
 
View attachment 2446256

Mwandishi wa habari wa TBC mkoani Manyara, Joachim Kapembe amefariki dunia Desemba 13, 2022 akishuka kutoka katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Kapembe aliungana na Waziri Nape Nnauye na viongozi wengine katika uzinduzi wa huduma ya intaneti kwenye kilele cha mlima huo.

Swahilitimes.

Kuna Siri gani Kati ya kishuka mlima Kilimanjaro na kifo?. Kuna rafiki yangu naye alifariki wakati wanashuka mlima Kilimanjaro.
 
Binadamu tunasema mengi Sana

Ndio siku Yao ishafika that's it

Ni kweli, lakini kila kifo kina sababu yake. Ndio nilitaka kujua Hawa wanaokufa wakishuka mlima Kilimanjaro hupatwa na Jambo gani?
 
Mlima kilimanjaro huwa na matabaka ya hewa tofauti, na hubadilika kila mara, wapandaji wanashauriwa jiandaa na kujitathimini kabla na wawapo safarini. Waeza panda ukifika mahali ka wajihisi vibaya bora kutoendelea

RIP
 
Back
Top Bottom