Mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), Azory Gwanda apotea. Ni siku 10 na hajulikani alipo

Mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), Azory Gwanda apotea. Ni siku 10 na hajulikani alipo

Inaumiza sana. Huyu mwandishi ni jamaa yangu wa karibu sana. Nimeshtushwa na hizi habari pia huyu ni mwana jf mwenzetu kabisa .

Wacha bana!!! anatumia jina gani humu? daah nouma kweli mi naenda Ifakara wameshavuna mpunga naenda kula pepeta na somba
 
2.jpg
Sikutegemea kuona nchi yangu iliyokuwa ikiongozwa na genius Kambarage kuwa mikononi mwa akina bashite
 
Mku sijakuelewa una maanisha nini ebu nielewishe kwani mm binadamu
Tafakari kwa kina mkuu, "soma katikati ya mistari".Ni kweli mpaka sasa haujajua hao waliomfanyia upekuzi na kuondoka nae ni wakina nani?
 
Tafakari kwa kina mkuu, "soma katikati ya mistari".Ni kweli mpaka sasa haujajua hao waliomfanyia upekuzi na kuondoka nae ni wakina nani?
Mku hii mambo ni hatari sana na haya yanafanyika Viongozi Wastafu na wa imani wako kipya. Nchi ni moja haya yanayifanyika watu wanayajadili na kupata majibu ambayo sio mstakabali mzuri kwa nchi yetu
 
Tukubali kuwa wananchi wa kawaida, blogers, wanasiasa, na wakosoaji wengine hawapo salama ktk Tz hii ya awamu ya tano. Lkn kwa nini iwe hivyo? mtu apotezwe bure bure tu na watu wasojuilikana? watawala wakumbuke kuwa histora hujirudia. Amerika ya kusini ilipitia enzi mbaya sana ya raia na wakosoaji wa tawala dhalimu na madikteta wote wa amerika ya kusini waliishia vibaya ama walipunduliwa ama waliishia ktk mahakama ya uhalifiu wa kivita. Historia na wakati ni mwalimu mzuri. Ktk leadhership kuna kuiga best practice ya aina ya viongozi wanaofanya vyema ktk kuongoza nchi zao. Lakn sisi Tz kwa bahati mbaya viongozi wetu wanaiga leadership approaches za Rwanda na Uganda na kusahau kuwa nchi hizi tatu zimepitia uzoefu tofauti wa kisiasa.

Inasikitisha sana kusoma kila siku ktk media kuwa eti huyu kapotea, huyu kapigwa risasa 32, huyo kafichwa na huyu kabinywa mapumbu na kutolea meno kwa pakari alimradi ni shida. Viongozi na watawala wakumbuke kuwa mazingira salama na kulinda haki za kila kundi ndyo njia pekee tutakayojenga Tanzania salama. Vitisho, mauaji na kupotea kwa wananchi wasio na hatia vinabomoa nchi. Abadan havijengi. Bila ya kuheshimu haki hakuna Amani( Rejea statements za Mr George Owel). wala tusijidanganye. Binadamu ni kama mpira. Kiwango cha uvumilivu kina mwisho pale maximum point of elasticity inapofikia ndo inakuwa mbaya zaidi kwa sababu anayeoonewa akivaa koti la mnyama anakuwa hatari na mbaya zaidi.

Wanaofanya vitendo hivi wasijisahau. Tz hakutakuwa na truth and reconciliation committee wakati mambo yatakapogeuka. Ubaya hulipwa kwa ubaya. Hatujazoea vitisho hivi ndo tunaviona ktk awamu hii. Naomba viongozi wa dini wasijifiche kama mbuni watoke mafichoni na wakemee uoza huu na sio kukaa kimya kama kwamba hakuna baya lolote. Akina Shiekh Mussa wa dsm, Kadinali Pengo na viongozi wengine wote. Nawapendeni na ninakuheshimuni sana lkn ifike wakati mpapai tuite mpapai na sio mgomba. Tumieni influence mliyonayo kuiwka tanzania sehemu salama.
Pengo na sheikh musa wote wanafiki wapo tayari kondoo wapotee mradi washibishe matumbo yao
 
Tafakari kwa kina mkuu, "soma katikati ya mistari".Ni kweli mpaka sasa haujajua hao waliomfanyia upekuzi na kuondoka nae ni wakina nani?

Mkuu nijuze ni akina nani hao wameondoka nae ama kumteka? daah Tanzania yetu ngoja niombe kwa Mungu kwa hisia kwanza
 
Vizuri uongozi MCL ,wametimiza wajibu wao.Tuviachie vyombo vya usalama vitatupa mrejesho.
 
Mku hii mambo ni hatari sana na haya yanafanyika Viongozi Wastafu na wa imani wako kipya. Nchi ni moja haya yanayifanyika watu wanayajadili na kupata majibu ambayo sio mstakabali mzuri kwa nchi yetu
Nimejitahidi kukuelewa hivyo hivyo tuu
 
Inabidi tuanze kuwa na utamaduni wa kunakili namba za magari (na picha pale tunapoweza) na kuwatumia watu wetu wa karibu pale tunapoitwa kwenye shughuli za dharura na hata kama tutaongozana na watu tunaowajua...
 
Back
Top Bottom