Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,292
- 10,842
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kilimanjaro, Gabriel Mwangosi amesema hakuna kitu kinachoitwa ‘Kodi Kubwa’ kwenye sheria za kodi bali kodi inayostahili.
Ameyasema hayo baada ya wamiliki wa shule mkoani Kilimanjaro kulalamikia makadiri makubwa ya kodi ambapo shule nyingi zinadaiwa kati ya Tsh Milioni 100 hadi Tsh Milioni 700 kwa baadhi ya shule.
Huku baadhi ya shule ambazo zinamilikiwa na kanisa katoliki zikitoa sababu kuwa hawafanyi biashara na kwamba madai hayo ya kodi yanaweza kuathiri uendeshaji wa shule.
Mwangosi amesema shule ambazo zinalalamika kupelekewa makadirio makubwa ya kodi, hazikupeleka taarifa zilizotakiwa TRA kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2016 hadi 2018 na kwa kutopeleka taarifa hiyo ni kosa.
===
Rungu la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika ukusanyaji wa kodi, limeziangukia baadhi ya shule za binafsi mkoani Kilimanjaro ikisemekana zinadaiwa kupelekewa madai ya kati ya Sh100 milioni hadi Sh700 milioni kila moja.
Baadhi ya wakuu wa shule hizo zikiwamo za Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi wamedai madai hayo ya kodi ni makubwa kwao na yataathiri kwa kiasi kikubwa uendeshaji wa shule hizo, zikidai zenyewe zinatoa huduma na hazifanyi biashara.
“Unajua sisi ni watoa huduma hatufanyi biashara, sasa Serikali ingeangalia makadirio ya kodi ambayo hayataathiri uendeshaji. Sisi tunasaidia Serikali kutimiza lengo la kutoa elimu kwa wananchi wake,” alisema mmoja wao.
Gazeti hili jana na juzi lilishuhudia baadhi ya wakuu wa shule wakiingia na kutoka katika ofisi za TRA Mkoa wa Kilimanjaro na inaelezwa baadhi waliwasilisha nyaraka kujaribu kuishawishi mamlaka hiyo kuwa madai yake si halisi.
Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Elimu Jimbo Katoliki la Moshi, Padre William Ruwaichi alisema kwa upande wa kanisa wanaendelea na mazungumzo na TRA na wanaamini mambo yatakwenda vizuri na yatakuwa sawa.
Jimbo Katoliki Moshi linamiliki shule 29 za sekondari, vituo vya mafunzo ya ufundi 15 na shule za awali na msingi 11 na taarifa kutoka ndani ya uongozi wa kanisa hilo zinadai shule zake za sekondari zilizoingia katika changamoto ya kodi ni tisa.
Kwa upande wake, mratibu wa elimu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Daniel Swai alisema kanisa limekuwa likijitahidi kuhakikisha kodi zinazotakiwa kulipwa zinalipwa.
Hata hivyo, baadhi ya wakuu wa shule za KKKT pia walilalamikia kupewa makadirio makubwa kuliko uhalisia wa mapato, madai ambayo Meneja wa TRA mkoa, Gabriel Mwangosi aliyakanusha akisema makadirio yao ni sahihi.
Ufafanuzi wa TRA
Mwangosi alisema katika sheria ya kodi hakuna kitu kinachoitwa kodi kubwa, na kwamba ipo kodi inayostahili ambayo inajengwa na misingi ya kumbukumbu na nyaraka ambazo zinathibitisha kuwa kodi ni kiasi fulani.
Kwa mujibu wa meneja huyo, makadirio ambayo pengine wamiliki wa shule wanasema ni kodi kubwa, ni malimbikizo yao ambayo waliyafanya kwa kutotekeleza sheria au matakwa ya sheria za kodi.
Mwangosi alisema shule ambazo zinalalamika kupelekewa makadirio makubwa ya kodi, hazikupeleka taarifa ambazo zilitakiwa TRA kwa kipindi cha miaka mitatu 2016 hadi 2018 na kwa kutopeleka taarifa hiyo ni kosa.
Meneja huyo alifafanua kuwa katika ukaguzi, walibaini shule hizo zilikata kodi kwa wafanyakazi (Paye) ambao ni walimu na kuitumia badala ya kuziwasilisha TRA kama inavyotakiwa kisheria.
Pia alisema kuna makato ya asilimia mbili ambayo shule ziliwakata watoa huduma waliowauzia bidhaa kama mahindi, maharage, mikate, mafuta na huduma mbalimbali ambazo wanapewa lakini hawakuziwasilisha TRA.
“... kodi ya taasisi ambayo ilipaswa ilipwe kutokana na faida, nayo haikulipwa na hizi zote ukizijumlisha ndiyo kodi ambayo ilikadiriwa. Kama mtu anaona ameonewa, yeye anapaswa kutoa kumbukumbu zake zinazoonyesha kipato chake,” alisema.