Huwa najiuliza hivi wanaume ukitoa hizo pesa na mali huwa mnataka mpendewe nini kingine, maana kama ni mionekano wengi mna mionekano ya kawaida ambayo haiwashitui wanawake na kama ni tabia ndio kabisa wenyewe tabia zenu mnazijua, utasikia "oo nataka unipende kama nilivyo" mbona hata ninyi huwa hamuwapendi wanawake kama walivyo ni either mtapenda mionekano au tabia nk
Huwa mnasema pesa na mali vinaisha kwani uzuri na mvuto ndio haviishi, tena binafsi naona bora hata yule ambaye anampendea mtu pesa maana zinatafutwa kuliko yule anayempendea mtu uzuri maana uzuri hautafutwi na binadamu hajiumbi, si kila mtu anapenda hayo ma surgery na ma make up maana mengi yana madhara tu
Na kingine ninyi wenyewe mkishawaweka ndani hao wanawake huwa mnachepuka kama mnavyosema wenyewe, mwanaume hatosheki na mwanamke mmoja hivyo tunaassume hakuna mwanaume asiyechepuka na ukiacha kuchepuka pia wengi ni walevi au wanywaji, hivyo mkitoka kwenye shughuli za utafutaji huwa mnaamua kukaa baa na washikaji hadi kupelekea kuchelewa kurudi nyumbani
Mara nyingi mnajikuta mnakosa muda wa kukaa na familia zenu either wake tu au wake na watoto, na wake zenu wakihoji huwa mna kauli zenu eti ninyi ndio mmetoa mahari hivyo mna haki ya kurudi muda wowote mnaotaka bila kuulizwa, mara sijui mnataka turudi mapema ili tukae tuanze kupiga umbea na kuangalia tamthilia mara oo kwani wewe humu ndani unakosa nini si unavaa, unakula, unalala na mahitaji yako mengine unapata sasa unataka nini
Mwisho wa siku mke anaona kwahiyo kumbe hivyo unavyompa (ambavyo ni pesa na mali) unaona ndio vya muhimu zaidi kwake kuliko uwepo wako, ndipo hapo naye anapoanza kujenga interest na mali zako zaidi kuliko wewe, na akiona unaendelea na tabia zako za kuchepuka na kuchelewa kurudi nyumbani hana budi kuvunja hiyo ndoa ili mgawane hizo mali maana wewe humpi muda wako