Mwanza: Baa ya The Cask yafungwa kwa tuhuma za ukwepaji kodi

Mwanza: Baa ya The Cask yafungwa kwa tuhuma za ukwepaji kodi

wabongo mkisikia swala la kodi moja kwa moja mnajua kodi ya mapato ya TRA wale wamepanga pale rock city mall inawezekana hawalipi kodi ya pango na ushuru mwingne ambao uko chini ya halmashauri

ivi mkurugenzi wa halmashauri akisema hawalipi kodi kwa miaka miwili mnafikiri kodi zipi ? kodi ambazo zipo chini yake

ila sema lile litakua figisu la ile video ya bandari
 
Huyo mwenye hiyo bar hana akili au anajuwa anachokifanya.
Kwa nini asiwe na akili?

Kuna sheria gani iliyovunjwa katika tukio hilo?
Na hata ingekuwa sheria imevunjwa, kwa nini ihusishwe na mambo ya siasa na hukumu itolewe kisiasa?

Inaonyesha wazi wew ndiye uliyepungukiwa akili.
 
Huko Mwanza TRA nao wemekanusha hawaidai Cask kodi yo yote.
Hii nchi hii mamlaka hukurupuka tu na ni kama hawana ukaribu au mawasiliano yo yote kabla hawajafanya maamuzi
IMG_4453.jpg
 
Mwigulu nchemba si alisema hakuna kufunga biashara? Sasa mtu anafungiwa biashara kwa kukwepa kodi sasa kwanini asilioishwe faini? Au kuna zaidi ya hili?
rais wa mawe na madaraja............upcoming Jiwe blessings
 
Mwigulu nchemba si alisema hakuna kufunga biashara? Sasa mtu anafungiwa biashara kwa kukwepa kodi sasa kwanini asilioishwe faini? Au kuna zaidi ya hili?
😎 😎 😎 😎 😎 Tunatafuta fedha za kumlipa Yap Markez
 
toka lini mkurugenzi akakusanya kodi ya TRA iyo kodi ni kodi ya pango wale wamepanga pale rock city mall mali ya halmashauri
Acha uchawa THE CASK haiwezi kushindwa kulipa hela ya pango! Kwanza hakuna utaratibu kama huo wa kufunga biashara ya mtu bila kutoa taarifa kwa mhusika! Na kwa nini ije sasa hivi baada ya kuonekana kwa ile Video? Nyinyi mchawa mda mwingine mnakosa hata akili!
 
Serikali wilayani llemela mkoani Mwanza imeifunga bar maarufu ya The Cask Bar & Grill jijini Mwanza kwa tuhuma za ukwepaji kodi kwa kipindi cha miaka miwili.

Kwa mjibu wa Mkurugenzi wa manispaa ya llemela Kiomono Kibamba, amesema uongozi wa bar hiyo umekwapa kodi ya Serikali na kuendesha biashara zaidi ya moja eneo hilo hilo.

Akizungumza katika eneo hilo la Bar Mkurugenzi wa llemela, Kiomoni Kibamba amesema mmiliki wake amekiuka masharti ya uendeshaji wa biasharaikiwemo kukosa leseni ya biashara kwa kipindi cha miaka miwili.

Pia soma:
- Imekuwaje The Cask Bar waombe radhi kwa wateja wao kuwa na ujumbe wa kuokoa bandari
Kukosa leseni kwa miaka miwili hilo ni uongo , Ushahidi huu hapa

Screenshot_2023-08-17-17-30-37-1.jpg
 
Serikali wilayani llemela mkoani Mwanza imeifunga bar maarufu ya The Cask Bar & Grill jijini Mwanza kwa tuhuma za ukwepaji kodi kwa kipindi cha miaka miwili.

Kwa mjibu wa Mkurugenzi wa manispaa ya llemela Kiomono Kibamba, amesema uongozi wa bar hiyo umekwapa kodi ya Serikali na kuendesha biashara zaidi ya moja eneo hilo hilo.

Akizungumza katika eneo hilo la Bar Mkurugenzi wa llemela, Kiomoni Kibamba amesema mmiliki wake amekiuka masharti ya uendeshaji wa biasharaikiwemo kukosa leseni ya biashara kwa kipindi cha miaka miwili.

Pia soma:
- Imekuwaje The Cask Bar waombe radhi kwa wateja wao kuwa na ujumbe wa kuokoa bandari
Mwambieni mmiliki apandishe hii bendera ya chama hapo bar figisu za machawa zitaisha
images-8.jpg

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom