Mwanza: Bwana harusi ajinyonga akisubiriwa ukumbini

Mwanza: Bwana harusi ajinyonga akisubiriwa ukumbini

Watu wanaendelea kukataa kuvuka mwaka 2022 jamani.
BTW, May his soul R.I.P
 
Bwana harusi ajinyonga akisubiriwa ukumbini

Mwanza. Sherehe ya harusi kati ya Swadiku Abas (50) na mke wake, Elieth Rwegashora (40) ambao ni wakazi wa Mtaa wa Zenze eneo lililopo Kiseke wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, iligeuka msiba baada ya bwana harusi kujinyonga muda mfupi
Safi sana. Bora wapungue tu angalau tule mara moja kwa siku.
 
Hii scenario imefanana na ile simuliza ya IBRA wa PILI kumuhusu John Ngweru wa Zimbabwe

Rip Maheremu
Pole kwa Marehemu
Pole kwa wafiwa, ndugu, jamaa na marafiki popote walipo
 
Huyu bwana harusi vp,kakumbwa na pepo gani sijui, all in all duniani mambo ni mengi na muda ni mchache
 
Swadika Abasi (50), mkazi wa Kiseke katika Manispaa ya Ilemela amejinyonga hadi kufa kwa mtandio sebuleni kwake baada ya kujifunga na kujining’niza kwenye kenchi la paa la nyumba yake.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Wibroad Mtafungwa alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 17, mwaka huu, saa 5.45, Mtaa wa Zenze, Kata ya Kiseke katika Manispaa ya Ilemela.

Alisema ilidaiwa Swadika alikuwa akiishi na mkewe aitwaye Elieth Rwegoshera (40) ambaye pia ni mkazi wa Kikseke-Ilemela waliyekuwa wametoka kufunga ndoa siku hiyo ya Desemba 17, majira ya saa moja katika msikiti wa Swadikil Amiin Kiseke.

Alisema baadaye walitarajia kwenda kufanya sherehe fupi katika ukumbi wa Mtena B ulioko Buzuruga. Hata hivyo, hadi saa nne usiku mwanamume huyo aliyekuwa akisuburiwa hakutokea ukumbini.

“Ilibidi sasa atafutwe na walipokwenda nyumbani kwake walikuta amejinyonga kwa mtandio huku mwili wake ukiwa umening’inia kwenye kenchi,” alisema.

Kamanda Mtafungwa alisema katika uchunguzi wa awali walipatikana kipande cha karatasi chenye ujumbe wa kujiua unaohifadhiwa kwa sasa kwa ajili ya upelelezi na uchunguzi. Hata hivyo, Kamanda hakutaja ujumbe huo ulihusu nini.

Aliwataka ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu kuwa watulivu wakati polisi wakiendelea na upelelezi wa tukio hilo.

“Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sekou Toure kwa uchunguzi wa kitalaamu,” alisema.
 
Kwa kweli stress ni mbaya sanaa..
Vyanzo vya huzuni ni vingi kuliko vyanzo vya furaha.
Pole yao wafiwa
 
Hii kali, inafikirisha na kusikitisha sana
 
Huyo mtu itakuwa kanyongwa na watesi wake...
 
Huyu jamaa kama kama namkumbuka wale mtaa wa zenze pls mwenye picha yake aitupie
 
Dah
Haya matukio yanaanza kuzoeleka sasa.

Polisi wachunguze
 
Back
Top Bottom