Mwanza City: The Photo Gallery

Ili jengo la abiria ni bora lingefanywa store tu hapo hamna kitu, archect aliyesanifu hili jengo nadhani hakuwa na exposure, jengo halina space ya kutosha, sehemu ya kutenganisha abiria wanaingia na wanaosafiri pia hakuna mtengano wa sehemu ya wageni pia na sehemu ya VIP, hili jengo ni ovyo sana nashauri lifanywe kuwa ghala la kuwekea mizigo au sehemu ya karakana, huyu msanifu ni mpumbavu sana nazani atakuwa ni the sunk fallacy cost huyu, hakika tumehujumiwa pakubwa.

Hatuwezi kuqualify kuwa international airport kwa hili pagale, hizo bilioni 13 walizozitupa kwenye hilo ghala la chakula ni bora barabara ya mkuyuni adi nyakato ingepigwa lami kwa hizo pesa.
 
Jengo la abiria aliendani na hadhi ya jiji la Mwanza, tunaomba TAA iangalie hili swala kama kutakuwa na upanuzi wa hili lijengo ili basi iweze kuwa terminal ya uhakika, tunaomba mamlaka husika itenge fedha zingine kwa ujenzi wa jengo bora la abiria na si hili ghala la mizigo.

Kwa tathimini za haraka ili jengo lina thamani ya bilioni tatu(3 bil) lakini utaambiwa ni bilioni 13, wahuni wamepiga kama bilioni 10.
 
Jengo hilo limejengwa kwa hela za mapato ya ndani ya ILEMELA na mwanza CC ,kwa kutumia force account bilion 4 zimetumika ...hapa ni haraka za Magufuli ndo zimetuponza ,,nadhani TAA wameliona hilo ndo maana wamewanyanganya halmshauri mradi huo ,,,,pia jaribu kupitia bajeti ya mwaka ya wizara ya ujenzi wamegusia ujenzi wa jengo hilo
 
Kumbe hili jengo lina thamani ya bilioni.4 na si 13? Na je hiyo bajeti imeongelea ujenzi mpya wa jengo la abiria au upanuzi?
 
Hili halistahili ata kuitwa terminal 1 ni bora likaitwa terminal 0, wajipange waanze ujenzi wa terminal 1 angalau liendane na hadhi ya jiji la Mwanza.
Serikali sijui iliwaza nn kujenga uwanja wa kimataifa songwe wakaacha mwanza ,,sijui Magufuli alikuwa na haraka gani kuruhusu ujenzi wa jengo lile kibahili ,,,na ndio maana hata barabara ya airport imejengwa kibahili hata taa haina ..
 
Serikali sijui iliwaza nn kujenga uwanja wa kimataifa songwe wakaacha mwanza ,,sijui Magufuli alikuwa na haraka gani kuruhusu ujenzi wa jengo lile kibahili ,,,na ndio maana hata barabara ya airport imejengwa kibahili hata taa haina ..
Japo miezi kama mitatu iliyopita wamefunga mataa mazuri sana kuanzia hapo airport adi eneo la kanisani, kona ya malaika beach.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…