Mwanza City: The Photo Gallery

Toka kahama to MZA ..nimegundua haya ...
Shinyanga town panazidi kupendeza na Kuna mijengo mirefu inajengwa . barabara zake ni classic na pasafi .kahama tayari haina ubavu wa kubattle na shinyanga kwenye suala la usmart ,mipango na miundombinu.kahama watabaki kwenye biashara labda mapato .japo kuwa Kwa ubora wa makazi na ukuaji kahama bado Iko juu.
Barabara ya kuanzia mpka wa mwanza na shy Hadi usagara ni viraka,makorongo,mashimo ,vifusi na vumbi (tanroads wakandarasi hawafanyi kazi )..ni barabara mbaya ya lami za mikoa nahisi kuliko zote ..
 
Usagara nimeipenda aisee .sa hv inataka kuungana na ukiriguru ,,,pale center pamekuwa smart ,daladala Costa za kwenda maeneo ya town ni nyingi ,,,panazidi kupendeza,,,naunga mkono hoja ya hili eneo kuondolewa misungwi ..
Nyegezi Ile niliyoiona kwenye video ya ngokongosha (kungurume).na hii niliyoiona live .hii ya live ni nzuri ,huko baadae patazidi kupendeza
Buzuruga bado Pako powa na stendi Ile Inatumika kama kituo Cha daladala na machinga .
Nyamhongolo ya kuiona live ni nzuri na kubwa kuliko picha tunazoziona mtandaonj...
Stendi ya nyegezi ni amazing [emoji91] nyamhongolo ni awesome [emoji91]
Hongera MCC , hongera ICC na JPM ..
jiji la mwanza limekua sana ,,, viongozi waache kulidharau .....
NB .nimepita tu nitarudi ijumaa ili nijionee vizuri
 



 

Attachments

  • Screenshot_20221129-221037_Instagram.jpg
    109.2 KB · Views: 7
  • Screenshot_20221129-220906_Instagram.jpg
    87.8 KB · Views: 7
  • Screenshot_20221129-220915_Instagram.jpg
    117.9 KB · Views: 7
  • Screenshot_20221129-220930_Instagram.jpg
    89 KB · Views: 7
Kisesa Pako hot ..chuo ,stendi ,geo position yake inaifanya ikue ,,Magu waelekeze nguvu zao hapa waipange ikae saw.. other wise itakuwa mji usio eleweka
Ukiachana na Rami kutoka Kisesa to Usagara, Hakuna chochote serikali hata ya halmashauri imeweka.

Stand mpya ipo IPO tu, ni watu ndio wanajenga frame za biashara.

In short, hiyo Kisesa inakuwa yenyewe tu haina mpangilio Wala utaratibu wa serikali.

Kwasasa watu wamejaa almost zaidi ya 70% ya Kisesa ni town, kuanzia Kisesa center, kuelekea Usagara, imejengeka mpaka Kuna sehemu wanaita Igekemaja.

Ukiingilia chuo Cha mipango ni mpaka mbele huko panaitwa Kigungumuli pako Moto.

Ukiingilia Bujora, mji umeenda mpaka huko mbele wanaita Mwahuli.

Hiyo Kisesa stand mpya yenyewe ukiwa Kama unaenda Kayenze mpaka Kassa zoo pako Moto sana.

Kwa uchunguzi wangu, nahisi Magu wameitelekeza Kisesa kutukana na HOFU ya kupoteza UWKEZAJI wao Kama Wilaya mpya ya Kisesa itakuja kuanzishwa. Lakini ili Kisesa iwe modernized town, Wilaya mpya haiepukiki.

Na nilivyoona, mji wa Kisesa kuelekea Magu umekuwa mpaka Nyanguge.

Na ikitokea kweli barabara ya Njia nne ikajengwa kutoka Mwanza CBD to Nyanguge, Basi Kisesa inakuwa imepata booster ya hatari sana.
 

Jiji la Mwanza kujengwa upya​



  • Wanaliita Jiji la Mawe (Rock City) kutokana na mwonekano wake wa kuzungukwa na milima yenye mawe mengi huku baadhi ya wakazi wakijenga nyumba zao kwenye miamba.

Mwanza. Wanaliita Jiji la Mawe (Rock City) kutokana na mwonekano wake wa kuzungukwa na milima yenye mawe mengi huku baadhi ya wakazi wakijenga nyumba zao kwenye miamba.

Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka huu yanaonyesha Mwanza ni mkoa wa pili kwa idadi kubwa ya watu ukiwa na zaidi ya watu milioni 3.69 nyma ya Dar es Salaam wenye milioni 5.38.
Sensa hiyo pia imeonyesha Mwanza ni ya pili kwa idadi kubwa ya majengo. Wakati Dar es Salaam ikiongoza kwa kuwa na nyumba 913,707, Mwanza zipo 868,430 na Dodoma836,909.

Hata hivyo, kutokana ongezeko la watu mkoani Mwanza, sura ya jiji imeanza kuharibika kutokana na makazi holela hali iliyolazimu kuandaliwa kwa mpango kabam be wa kulijenga upya jiji hilo kwa ushirikiano wa Serikali na sekta binafsi (PPP).
Akitoa mada katika Jukwaa la Maendeleo Endelevu (GGP) uliojadili usimamizi madhubuti wa fukwe kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii hivi karibuni, Ofisa Mipangomiji wa Jiji la Mwanza, Evodia Kisoka amesema kutakuwa na maboresho ya ufukwe wa Tampere ambao ni miongoni mwa zinazomilikiwa na Serikali, nyingine ni Kamanga.
Fukwe zinazomilikiwa na watu binafsi mkoani humo ni Faulu, Jembe ni Jembe, Waghill, Rock Beach, Kishimba, Kapricabana, Tamali, Sunset, Shafick Meral na Havash.

Ufukwe wa Tampere
“Ufukwe wa Tampere upo mkabala na jengo la Benki Kuu ya Tanzania ambao unaanzia Mto Milongo na unaambaa hadi kona ya Kirumba. Ukubwa wa eneo ni hekta 9.30,” anasema Kisoka.
Ofisa huyo anasema mpango kabambe (master plan) wa Jiji la Mwanza wa mwaka 2015 hadi 2035 unaonyesha ufukwe wa Tampere utakuwa na jengo kubwa litakalokuwa alama ya Mwanza.
“Katika eneo hilo, maji ya ziwa yatasukumwa na kutengeneza ras ambako kutajengwa jengo refu ambalo ni alama (iconic building) ya utambulisho wa Jiji la Mwanza,” anasema.

Katika eneo hilo, anasema kutakuwa na alama nyingine mbili, kusini kutakuwapo beacon ambayo ni alama ya ufuatiliaji (police patrol and watch tower) na upande wa kaskazini kutakuwa na jengo litakalotambulisha shughuli za majini.
Miradi mingine, Kisoka anasema ni michezo ya watoto, miundombimu kwa ajili ya watu kupumzika, eneo la michezo ya ufukweni na burudani, na mapishi ya samaki kama vile kuoka na kubanika.
Akieleza faida za mradi huo, Kisoka anasema wananchi watapata sehemu nzuri yenye madhari yenye hewa safi kwa ajili ya kupumzika na michezo.
“Kutakuwa na fursa za kiuchumi kwa wajasiriamali na kimazingira, eneo litakuwa na madhari nzuri ya kuvutia,” amesema.
Hata hivyo, anasema kwa muda mrefu maeneo hayo yamekuwa hayafikiki kirahisi kutokana na ubovu wa barabara ndio maana kuna mpango wa kuendeleza fukwe kudhibiti uchafuzi wa mazingira kutokana na utupaji taka ovyo.
Kisoka anasema Halmashauri ya Jiji la Mwanza inakusudia kuingia ubia na sekta binafsi kuuendeleza ufukwe huo.
“Ufukwe wa Tampere unatoa fursa kwa wawekezaji wakubwa, wa kati na wadogo kutoka ndani na nje ya nchi kuwekeza kwa kujenga hoteli, maduka makubwa, ya kati hata ndogondogo.
“Alama ya utambulisho wa Jiji la Mwanza itakuwa kivutio kwa watalii wa ndani na nje. Wakazi wa Jiji la Mwanza na wageni watapata fursa ya kufanya utalii wa ufukweni,” anasema.
Akifafanua kuhusu mpango huo utakaogharimu Sh3 trilioni, Ofisa Mipangomiji wa Mkoa wa Mwanza, Misana Bihemo anasema wakati wanautengeneza waliangalia unakoelekea mji.
“Mwanza imezungukwa na milima ambayo ni kikwazo cha ukuaji wa mji, kwa hiyo inatoa mwelekeo wa kwenda ziwani ndiyo maana tunafanya reclamation (utengenezaji wa rasi) inayotegemea ripoti za mazingira, kama itashindikana itabidi tupunguze miradi kutoka 25 hadi 22,” anasema.

Mpango huo pia unakusudia kuboresha makazi ya wananchi waliopo milimani.
“Hatuwezi kuwa na mpango huu halafu watu waendelee kuwa pale milimani. Unajua hadi mtu anakwenda pale, anakuwa na sababu zake, inawezekana ni urahisi wa usafiri wa kuja mjini. Kwenye mpango huu tutafanya maboresho ya makazi ingawa watu watabaki palepale,” anasema.
Akifafanua kuhusu hilo, Bihemo anasema kwenye eneo la mita za mraba 100 kunaweza kuwa na nyumba 50 hivyo pakijengwa ghorofa patakuwa salama zaidi likipita tetemeko la ardhi.
Bihemo aliyeshiriki kuandaa mpango huo, anasema kuna miradi 25 katika eneo hilo lakini wataanza na mitano ambayo ni kichocheo ili izalishe fedha za kujenga mingine.

Uzoefu wa NSSF
Akizungumza katika eneo litalojengwa mradi huo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Profesa Godius Kahyarara ameshauri ushirikishwaji wa kutosha kuepusha mgongano utakaochelewesha utekelezaji.
Profesa Kahyarara aliyewahi kuwa mkurugenzi mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ametoa mfano wa mradi wa nyumba za Dege uliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam ambao sasa unatafutiwa mwekezaji mpya.
“Kwa mfano ule mradi wa Dege, sijui kama mliona mpango wake, sasa hivi tunatafuta mteja wa kuja kuununua. Kwa hiyo msichukulie kirahisi, mjue na mwekezaji akija ana matamanio yake. Mtu pesa anayo lakini huu mchoro hautaki, mnafanyaje?” alishauri.
Huku akitoa mfano wa mradi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Profesa Kahyarara pia ameshauri kuwa na miradi kama hiyo haipaswi kuwekwa kiporo inapoanza.
 
Mpango ni mzuri ila utekelezaji wake lazima uwe wa kusuasua tu.
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nikitafuta hardcopy ya masterplan ya mwanza.
Inaonyesha hili eneo linavyotakiwa kuwa mpaka mwaloni.
Kitana ni mtu wa hovyo sana, amejenga pale kwa ubabe ila masterplan haimruhusu.
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nikitafuta hardcopy ya masterplan ya mwanza.
Inaonyesha hili eneo linavyotakiwa kuwa mpaka mwaloni.
Kitana ni mtu wa hovyo sana, amejenga pale kwa ubabe ila masterplan haimruhusu.
Porojo tu wanaleta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…