KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Barabara hiyo ni muhimu na inatumiwa na Wanafunzi kwa asilimia kubwa kwa kuwa ipo karibu na Shule za Msingi Nyabulogoya na Nyegezi pamoja na Shule ya Sekondari Nyabulogoya.
Mbali na barabara hiyo kuharibiwa na maji ya mvua ila Wananchi wakitaka kujitolea kufanya ukarabati wa barabara hiyo, viongozi wa mtaa wamekuwa wakiwakataza na kusema ipo bajeti ya ukarabati wa Barabara, wanatoa kauli hiyo tangu Julai 2024.
Hii sio sawa, inabidi suala hili lifanyiwe kazi kwa kuwa linatuumiza wengi na linaathiri hata shughuli zetu za kiuchumi.
========================
UFAFANUZI WA SERIKALI YA MTAA
JamiiForums imewasiliana na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Chenga, Kata Nyegezi, Venance Edward Msinga kuhusiana na suala hilo, anafafanua:
Changamoto hiyo tunaifahamu na tumeiwasilisha kwa Vyombo husika, TARURA, ambao walisema kuna mafungu ya bajeti ya hilo suala yanakuja Januari (2025) sijajua imefikia wapi.
Pia tunatarajia kuwa na kikao na Mkuu wa Wilaya, tutaitumia nafasi hiyo kuzungumza suala hilo pamoja na Diwani kwa kuwa ni suala la muda mrefu.
Kuhusu Serikali ya Mtaa kuzuia Wananchi kufukia au kushughulikia barabara hizo mbovu, hatujawazuia kufanya kitu kama hicho.