Mwanza imezizima wananchi wakesha kuusubiri mwili wa mpendwa wao hayati Magufuli utakaowasili saa 1:00 asubuhi!

Mwanza imezizima wananchi wakesha kuusubiri mwili wa mpendwa wao hayati Magufuli utakaowasili saa 1:00 asubuhi!

Mtu anayekubalika huitaji kumpigia kelele zote hizi, ukiona mtu anajisifu/kusifiwa kuwa anakubalika/kupendwa jua kuna tatizo sehemu. Leo nimesikia eti wanampamba kuwa alikuwa mtu wa haki....nkasema mhuuuu jamani tumfika huko!!!

Na wewe mtazamo wako usilazimishe kuwa mtazamo wa wengine pia. Acha wanaoona alikuwa mtu wa haki waseme na wewe ruksa kuwa na mtazamo tofauti na wao.Kila mtu ana haki ya kutumia haki yake.
 
Hahahaaaa...... Niko kwenye msafara wa chifu Mareale bwashee tuna kibali cha kuingia hadi Chato siku ya Ijumaa, usimchukulie kizembe zembe bwashee!
Kumbe unatokea kwenye ukoo wa kichifu? Hongera sana mkuu [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Huo n udhalilishaj kwa marehemu wala sio upendo.
Waafrika tunafanyaga yale yale kila siku.
Pesa ya kuuguza kidogo,pesa ya kuandaa mazishi kubwa.

Trump alkuwa sahihi,hizi nchi zetu znatakiwa kutawaliwa tena.
Kwa jinsi dunia inavyoenda speed,hatukupaswa kutumia muda wote huo kwenye mwili wa baridi.
Unataka tumzike mapema kwani anawai kwenda wapi? Tunamuazima only 3 to 5 days ya maisha yake ya milele ebu mtuache na kipenzi chetu.
 
Sijapata kuona heka heka za kiwango hiki katika jiji la Mwanza ambapo watu wamekesha kumsubiri mpendwa wao hayati Magufuli waweze kutoa heshima za mwisho.

Kwa kweli hayati Magufuli anakubalika kanda ya ziwa maana nimeshuhudia wageni kutoka pembe zote za kanda hii wakiwa tayari kumpokea, kumuaga na hatimaye kumsindikiza hadi Chato kipenzi chao.

Vituo vya mafuta viko busy kuuza maana kila mmoja ameshakaa mkao wa mapokezi, kuaga kisha msafara kuelekea Chato baada ya zoezi la kumuaga hayati Magufuli kukamilika katika uwanja wa CCM Kirumba.

Updates;
Uwanja wa CCM Kirumba umefurika, watu ni wengi kweli kweli na wote wakiwa na sura za huzuni na simanzi.

Kule kwenye mzunguko ambako wamekaa wananchi wa kawaida kulijaa tangu alfajili kabisa kadhalika jukwaa la viongozi limeshasheheni wahusika.
Hivi wasukuma wanajuaga kuwa kila zama na kitabu chake?
 
Back
Top Bottom