Mwanza JF users: Tuunde umoja/utambuzi wetu


Uliyoongea ndiyo msingi wa umoja wetu kuwa ni wa hiyari, tuna katiba na viongozi. Mtu anayekuja kubeep hatuna shida naye na hatu maintain u star. Kila member ni sawa na mwingine hata kama na rep kiasi gani jukwaani.

Kwa misingi hiyo tumefanikiwa sana mpaka saizi na hilo tunashukuru Mungu japokuwa kuna watu wanatuona kama tunajichora lakini hilo linabaki kuwa changamoto kama siyo kulitupia mbali wazo au mtazamo kama huo.
 
Last edited by a moderator:
Daima changamoto zipo, cha msingi ni kusimamia azma hata kama una/utabezwa (hiyo ni sehemu ya jamii).
Umenena vema na vilivyo, tunasonga mbele.
 
tuanze kujisajili wapi ili tuanzishe record?
tujuane, tue kama lile kundi imara mwanza kwny facebok la
MWANZA NDIYO HOME
kweli wanasaidiana mawazo, ushauri, pesa nk
 
Hata sijui mkuu.... Hatujapanga kwenda huko ila mambo yatakapo kuwa tayari tutawajulisheni ni lini na wapi tukutane. Pia ni vyema ikawa wakati wa jioni kabla ya saa 3 usiku make wengine huenda wakashindwa kuhudhuria sababu ya muda.

kumbe na wewe ni wa mwanza dada,tuko pamoja kwa lolote unishirikishe
 
Umoja ni mzuri, tatizo nililonalo kwa umoja mingi ya waTZ inaishia kwenye mambo ya kuzikana, harusi vipaimara na mengine kama hayo. Binafsi nataka umoja wa mambo ya maemdeleo ya kiuchumi, yaani kunyanyuana kimaisha. Na hii najua ni ngumu sana kwa waTZ walio wengi, ndio maana JF Saccos niliiunga sana mkono lakini ndio ikawa vile tena.

all the best wa Rock City
 
tuanze kujisajili wapi ili tuanzishe record?
tujuane, tue kama lile kundi imara mwanza kwny facebok la
MWANZA NDIYO HOME
kweli wanasaidiana mawazo, ushauri, pesa nk

Juu ya venue/lini tutakutana, TUTAWAJULISHA. Let's get ready juu ya hili mkuu.
 

Thanks chief,
Tatizo la JE saccos lilitokea katika masuala ya usajili wa Saccos hiyo, ambapo tuliwahi kumualika (kama sikosei) msajili wa Saccos wilaya ya Kinondoni na alifika na kutuelimisha. Kulikuwa na tatizo la uongozi na kulaumiana, maana viongozi walikuwa ni wenye safari nyingi pasipo utulivu na ufatiliaji ulio wa karibu zaidi.
Kwa wale members wa JE Saccos nadhani huwa tunawasiliana sana kwa email especially kwenye kukumbushia uhai wake na uhai wa michango yetu (fedha) ya uanzishwaji wake.
Umoja huu tunaoutarajia kuuanzisha hapa Mwanza utaendana sana na mawazo ya members juu ya nini tufanye kama kikundi.
 

Mkuu sio lazima kubadilishana namba za simu. Kama mtu hayuko tayari kutoa namba zake na hata personal info ni sawa. Twaweza tumia PM na thread kujuzana vitu vitakavyokuwa vinaendelea ndani ya umoja huu.

Asante
 

Asante kwa mchango wako, nitakutafuta PM kwa ufafanuzi mahali fulani ambapo sijapaelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…