Home First
JF-Expert Member
- Feb 23, 2013
- 609
- 247
JF Rock City tupo wengi sana tu, ila wengi ni waoga sana kukutana.
Kuna wanaosema kuonana ni "Unafiki" n.k. Kwani Wing zingine huwa wanafanyaje na sie tushindwe? Kumekuwa na Umoja na Mshikamano miongoni mwa member waliokutana mpaka wana Wenyeviti na Makatibu Mf. JF Arusha Wing, je wao wanakabiliana vipi na huo unafiki? Je wanashindwa kukosoana wanapokosea ndani ya JF?
Wanaosema hakuna tija kufahamiana... Hamkuona kilichofanyika JF Arusha Wing kwa kwenda kutoa mkono wa pole kwa Dada yetu KOKUTONA? Wale tulioshiriki kwa namna moja ama nyingine tuliweza kutambua umuhimu wa JF na dada zetu kama Madame B, Smile, KOKUTONA na wengine wanaufahamu umuhimu wa JF.. wanaweza kuwa mashahidi hapa.
Hakuna haja ya kufahamiana kwa majina halisi labda ikitokea nikakutana na wewe Rock City kisha nikatambua kuwa wewe ndiye Boss wangu potelea mbali, ila tutambuana kwa ID zetu za JF.
Katika party iliyofanyika mwanzoni mwa mwaka huu "White Party" kuna watu waliohudhuria kwa kuficha ID zao. Kama hutotaka kujulikana unaweza kuficha ID yako. Si lazima tukufahamu kwa ID yako kama hutotaka.
Ni mawazo yangu....
Naunga mkono hoja,
Elewa kuwa huwezi kubalika na wote hata tukianza wachache watakaoona umuhimu watafuata.
Endelea kuangalia wangapi wamekubaliana nawazo lako kisha tupange tarehe na wakati wakukutana na mahali gani.
nihilo tu kwaleo.
Last edited by a moderator: