KERO Mwanza kuwa na changamoto ya maji ni aibu kubwa sana kwa jiji lenye vyanzo vingi vya maji kama hili

KERO Mwanza kuwa na changamoto ya maji ni aibu kubwa sana kwa jiji lenye vyanzo vingi vya maji kama hili

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

johnmashilatu

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2010
Posts
1,263
Reaction score
1,753
Nakariri maneno ya Hayati Robert Nesta Berhane selasie Malery alisema katik Rat Race " I abudance of water the fool is thirsty".

Kwamba mji wa Mwanza ulioko pembezoni mwa Ziwa victoria, likisemwa la tatu kwa ukubwa duniani na ambalo linatiririsha maji yake kupitia Ethiopia, Sudan hadi Misri lakini wakazi wake wanalia kiu!

Kwa hakika Bob Marley aliona mbali sana. Kwamba wakati maji hay yakisafirishwa lwenda shinyamga, Kahama Nzega, Tabora na nk, wakazi wa mwanza wanalia kiu.

Kwamba, kwa zaidi ya mwezi mmoja ya wiki mbili wakazi wa Bulale, kata ya buhongwa, hawajaona tone la.maji huku mamlaka ikituma "bill" za maji

Kwamba, wakazi hawa watiifu lwa taifa lao wanao9shi km tatu kutoka ziwani, hulazimika kuamka saa tisa usiku kwenda kwenye visima.na madimbwi kutafuta maji yanayokatika ifikapo saa tano asubuhi!

Kwamba, huyu " fool" kwa mujibu wa Bob Marley, hawezi kupaza sauti au kuwafuata wanaohusika kudai uwajibikaji!

Kwamba, katika zama hizi watu wanoishi pembeni ya ziwa wanalipa shilingi elfu tano ili kupata ndoo 10 za maji, huku wasiokuwa na uwezo wakiwa hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kwa kukosa maji!

Kwamba, baadhi yao, wenye " uwezo" na pengine " ubinafsi" wanaongelea kuchimba visima kwenye makazi yao, badala ya kudai uwajibikaji ili jamii yote ipate maji!

Nami nimalize na swali la Yesu kwa wagalatia "enyi watu wa Mwanza ni nani aliyewaloga?
 
Dah huwezi jua labda ndiyo wanaamini maisha yanatakiwa kuwa hivyo.

Ni kama vile kuna watu wanaamini ishu yoyote inayomfaidisha mtu wa kiwango cha kati mpaka chini haitakiwi kuwa vizuri. Zile vurugu na kucheleshwa kwa mabus ya mwendokasi watu wanaamini wanastahili kwasababu hawana magari.

Niliona kule X ililetwa story ya Capri point na nyumba maeneo hayo ambayo imekuwa ikitumika kwa mateso ya watu.

Nikaona kwa jinsi vile watu wanachangia unaona kabisa wanajua na wamekubali ile hali. Wanasiasa wanaenda kila siku, mitandao ipo ila wanatulia mpaka mtu wa mbali kabisa azungumzie shida ndiyo wataanza kulalamika.
 
Hii tabia ya kuamini kwamba matatizo yetu ama yataonddoka yenyewe au kuwasubiri akina "fulani" ndio wachukue hatua inatugharimu san kama nchi

Haiingii akilini, wakazi wa jiji la.Mwanza wakose huduma muhimu kama.maji kwa zaidi ya mwezi na nusu na hakina kinachotokea!
 
Mradi wa maji ya ziwa Victoria si unaanzia huko, ccm haikuwatandazia mabomba?
Hawa wakazi wa jiji hilo la miamba wanafurahisha, eti maji yanatoka kwao kwenda mikoa na nchi nyingine? Ilihali wao wana kiu. Sawa na ustaarabu wa mshumaa!
 
Hii tabia ya kuamini kwamba matatizo yetu ama yataonddoka yenyewe au kuwasubiri akina "fulani" ndio wachukue hatua inatugharimu san kama nchi

Haiingii akilini, wakazi wa jiji la.Mwanza wakose huduma muhimu kama.maji kwa zaidi ya mwezi na nusu na hakina kinachotokea!
Iko hivyo mkuu
 
Kila nikifika mwanza najiuliza...mgao wa maji unatoka wapi?...
Kuna kipind unakaa wiki maji hayatoki...viongozi wajitafakari sana
Kipindi cha Magu si serikali waliweka 700B kwenye ishu ya mradi wa maji huko.

Sijajua wamefikia wapi siwezi kuongea sana sijafika hayo maeneo
 
Kila nikifika mwanza najiuliza...mgao wa maji unatoka wapi?...
Kuna kipind unakaa wiki maji hayatoki...viongozi wajitafakari sana
Imawezekana viongozi wana mchango, lakini hao viongozi wanafikishwa na nani hapo walipo?hup uongozi mi mali yao? Wenye mali wako wapi?
 
Kipindi cha Magu si serikali waliweka 700B kwenye ishu ya mradi wa maji huko.

Sijajua wamefikia wapi siwezi kuongea sana sijafika hayo maeneo
Inaweza kutangazwa hata kuwekezwa Trilioni, lakiji kama wenye fedha na wenye maji na wenye kuwawajibidha hao viongozi, hawachukui hatua tatizo litaendelea.
Kwani si miezi.michache tu walisema wamezindua mradi.mkubwa eneo la.butimba na kwamba tatizo la.maji litakuwa historia?
 
Back
Top Bottom