Nakariri maneno ya Hayati Robert Nesta Berhane selasie Malery alisema katik Rat Race " I abudance of water the fool is thirsty".
Kwamba mji wa Mwanza ulioko pembezoni mwa Ziwa victoria, likisemwa la tatu kwa ukubwa duniani na ambalo linatiririsha maji yake kupitia Ethiopia, Sudan hadi Misri lakini wakazi wake wanalia kiu!
Kwa hakika Bob Marley aliona mbali sana. Kwamba wakati maji hay yakisafirishwa lwenda shinyamga, Kahama Nzega, Tabora na nk, wakazi wa mwanza wanalia kiu.
Kwamba, kwa zaidi ya mwezi mmoja ya wiki mbili wakazi wa Bulale, kata ya buhongwa, hawajaona tone la.maji huku mamlaka ikituma "bill" za maji
Kwamba, wakazi hawa watiifu lwa taifa lao wanao9shi km tatu kutoka ziwani, hulazimika kuamka saa tisa usiku kwenda kwenye visima.na madimbwi kutafuta maji yanayokatika ifikapo saa tano asubuhi!
Kwamba, huyu " fool" kwa mujibu wa Bob Marley, hawezi kupaza sauti au kuwafuata wanaohusika kudai uwajibikaji!
Kwamba, katika zama hizi watu wanoishi pembeni ya ziwa wanalipa shilingi elfu tano ili kupata ndoo 10 za maji, huku wasiokuwa na uwezo wakiwa hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kwa kukosa maji!
Kwamba, baadhi yao, wenye " uwezo" na pengine " ubinafsi" wanaongelea kuchimba visima kwenye makazi yao, badala ya kudai uwajibikaji ili jamii yote ipate maji!
Nami nimalize na swali la Yesu kwa wagalatia "enyi watu wa Mwanza ni nani aliyewaloga?