Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limemtia mbaroni mama mmoja aitwaye Happyness Mafuru, kwa tuhuma ya kuwatelekeza watoto wake wawili katika majaluba ya mpunga, huko mtaa wa Mtakuja kata ya Nyamhongolo wilayani Ilemela Jijini Mwanza.
Watoto hao wameokotwa wakiwa hai na kisha kupelekwa katika hospitali ya rufaa ya kanda Bugando Jijini Mwanza, ambako wanaendelea kuchunguzwa afya zao wakati uchunguzi dhidi ya tukio ukiendelea.
Watoto hao wameokotwa majira ya saa tisa usiku, huku baridi ikiwa ni yao na usalama ukiwa ni tishio la maisha yao, kama anavyosimulia Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mtakuja Adamu Magina.
============
Ni dhahiri kuwa wapo wanaohitaji watoto lakini hawajabahatika kuwapata, na waliobahatika wanashindwa kushukuru kwa kupata bahati hiyo ya mtende, lakini Je, ni hatua zipi zitafuata kwa Happynes na mumewe?
Kwa wenye kufahamu majaluba ya mpunga, katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha nchini majaluba mengi yamejaa maji, hivyo unaweza kupata picha, jinsi watoto hao walivyokuwa wakikabiliwa na wakati mgumu kunusuru uhai.