John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Diana Bundala maarufu kama 'Mfalme Zumaridi' na wenzake 84 leo Alhamisi Machi 17, 2022 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza kusomewa maelezo ya awali katika mashtaka matatu ikiwamo usafirishaji haramu wa binadamu.
Makosa mengine ni pamoja na kusanyiko lisilo na kibali na kuzuia maofisa wa Serikali kutimiza wajibu wao.
Tofauti na alivyokuwa akifikishwa awali Mahakamani hapo alipokuwa akijiachia na kuwatania waandishi wa habari hasa wapigapicha, akijiita Mungu, safari hii ilikuwa tofauti ambapo akiwa ndani ya Mahakama alijifunika kwa kitenge wakati akipigwa picha na kuziba uso wake.
Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo saa 6:00 mchana mbele ya ya Hakimu mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Monica Ndyekubora.
Mchungaji huyo kutoka Mwanza amepata umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii Instagram na YouTube akionekana anacheza huku baadhi ya video zikimuonesha ‘akisujudiwa’ na waumini wake.
Ni nadra sana kwa mwanamke kutumia jina ama cheo cha mfalme bali ni malkia, lakini kwa mchungaji huyu anaitwa kwa cheo hicho.
Diana Bundala maarufu kama 'Mfalme Zumaridi' akiwa amejifunika kitenge ndani ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kusomewa hoja za awali za mashtaka matatu yanayowakabili na wenzake. Picha na Mgongo Kaitira
Source: Mwananchi
Pia Soma>>>