Mwanza: Ukivaa nguo ya CHADEMA au yenye Maandishi "Katiba Mpya" huruhusiwi kuangalia mpira wa Simba na Yanga

Mwanza: Ukivaa nguo ya CHADEMA au yenye Maandishi "Katiba Mpya" huruhusiwi kuangalia mpira wa Simba na Yanga

WADAU Tanganyika kuna VIOJA
Uwanja unapochezewa Mechi ya SIMBA na YANGA umeandikwa CCM KIRUMBA
baadhi ya Watazamaji wa Mpira wa leo baina ya SIMBA na YANGA wamevaa Tshirt za Chadema
Jeshi la Polisi limewazuia Kuingia Eti Wanaleta SIASA Tafsiri ambayo wamejitoa Jeshi la Polisi.
CCM ndio inaleta SIASA ule Uwanja haukujengwa na CCM ulijengwa kwa Michango ya Wananchi wote bila kujali ITIKADI zao lakini kwa Kuwa CCM inaleta SIASA kwenye Kila kitu Wakauita ule UWANJA wa CCM KIRUMBA.
Jeshi la Polisi jaribu kuwa na Busara kumzuia Mtu kuingia Uwanjani wakati Kiingilio Kajilipia Sio Sahihi Tafsiri ya kuwa Kuvaa Tshirt ni SIASA hiyo ni yenu Jeshi la Polisi.

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Hayo yanasababishwa na kua na utindio wa kufikiri.Neno katiba mpya sio jinai nawala sio siasa ni mahitaji ya nchi sasa kinachowasumbua polisi wa hii nchi ni kipi hasa.mbona kama wanajiaibisha sana.Alafu wanakomaa na huo ujinga siku rais akisema anaanzisha mchakato wa katiba mpya utawaona tena wanavyotoa macho.Ukiwa mlinzi alafu hutumii akili ata ulinzi unaoufanya unakua hauna maana.
 
Hapo wameingia uwanja tu wa mpira. Ingekuaje kama mtu angeenda kituo cha polisi akiwa amevaa gwanda la CHADEMA?
 
Lakini sasa kwenye mpira na hayo mabo ya katiba mpya wapi na wapi jamani?
Kwani walienda kufanya vikao vya kuhusu katiba mpya uwanjani au ni nguo walikua wamevaa?.Kama tukianza kua na akili ndogo za kuogopa maandishi ambayo sio matusi basi tutakua taifa la ajabu.
 
Lakini suala la katiba mpya siyo ajenda ya wanachadema pekee. Ni hitaji la wananchi wengi bila kukali itikadi za vyama vyao ili mradi kila mmoja na namna yake ya kutafsiri mambo.
 
Back
Top Bottom