Mwanza: watoto waliotekwa wapatikana, watekaji wauawa kwa kupigwa risasi

Mwanza: watoto waliotekwa wapatikana, watekaji wauawa kwa kupigwa risasi

Inamaana hao watekaji hawana ndugu ama sio watanzania?

JF hakuna members aliye mitaa ya watejaji watupe stories za hao watu!
Ngoja tufuatilie uwepo wa miili kwanza, wakikaza basi. Ile hii story ina walakini,acha tuafauatilie kidogo huwezi jua
 
Amani iwe nanyi wapendwa

Wale watoto waliotekwa hatimaye wamepatikana lakini watekaji wameuliwa.

=====

View attachment 3229443

Wanafunzi wawili wa Shule ya Blessing Model School waliokuwa wametekwa na watu wasiojulikana Februari 5, 2025 jijini Mwanza wamepatikana huku watekaji wakipigwa risasi na kupoteza maisha baada ya kuonesha nia ya kutaka kuwashambulia maaskari wakiwa na silaha.

Akizungumza katika eneo la tukio Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema watoto hao wamepatikana wakiwa wamefichwa katika nyumba namba 8 iliyopo katika Mtaa wa Nyagoloboya Kata ya Nyegezi huku watekaji wakiwa humo.

Pia soa > Mwanza: Watoto wawili wa Shule ya Blessing Model watekwa, wengine Wanne wanusurika

Hata hivyo Kamanda Mutafungwa amesema baada ya maofisa wa jeshi hilo kuzingira nyumba na kuwataka watekaji watii amri walitoka wakiwa na silaha kama mapanga na rungu hali iliyopelekea kutumia risasi.
ACP Mtafungwa aongeze task forces huu mji unaokena kuwa na matukio mengi na ajabu ajabu sana. Asiwalee kabisa asafishe jiji bila kuangalia usoni.
 
Nadhani Mpaka sasa sio wasiojulikana.Watoto wamepatikana wakiwa salama hongera sana.
 
Hata hivyo Kamanda Mutafungwa amesema baada ya maofisa wa jeshi hilo kuzingira nyumba na kuwataka watekaji watii amri walitoka wakiwa na silaha kama mapanga na rungu hali iliyopelekea kutumia risasi.
Hii nadhani ilikuwa ni amri lazima wauawe

Kinyume cha hapo uwezekano wa kuwapata wakiwa hai ulikuwepo sababu wahalifu hawakuwa na siraha za moto

Mapanga na Rungu wangeweza kudhibitiwa na askari mmoja tu mwenye mafunzo

Amri iliyotoka hawakupaswa kuishi, huu ni utaratibu unaotumika kwa waharifu sugu,
Ukikamatwa mara ya kwanza watakuonya uachane na uharifu ukizingua mara ya pili wanakupoteza

Kuna mtu mzito nyuma ya wahalifu hivyo endapo wangekamatwa na kubanwa wangemtaja hivyo vyovyote vile ni lazima wauawe
 
Kuna jamaa/msikilizaji pale magic fm, alikua akipiga simu na kusema polisi na majambazi lao moja, ulikua mjadala,hadi hali ilipokua dhahiri
Huyo anajua uhalifu wa baadhi ya polisi wala hakuwasingizia. Tukio la wafanyabiashara wa madini toka Mahenge, Morogoro kama si rais Kikwete kutaka uchunguzi ufanyike basi watu wangeendelea kuamini porojo za polisi kuwa walikuwa majambazi kumbe ni uongo.
 
Wangekuwa wezi wa kawida sawa utawapeleka kwa hakimu wakajitetee, lakini unateka vitoto kisha unataka wapelekwe polisi kama bibi na bwana harusi !! hapana.
Chapa risasi tu mambo yaishe.
Taarifa za polisi si za kuamini bila kuhoji. Mwaka 2006 polisi waliwaua wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, Morogoro na dereva taxi na kutangaza kuwa walikuwa ni majambazi. Ndugu wa wafanyabiashara hao wakakataa kuwa ndugu zao hawakuwa majambazi na wakamuomba rais Kikwete afutilie sakata hilo. Baada ya rais kuunda tume ndipo ikabainika kuwa watu wale hawakuwa majambazi na hawakuwa na shtaka lolote la kihalifu.
 
Huyo anajua uhalifu wa baadhi ya polisi wala hakuwasingizia. Tukio la wafanyabiashara wa madini toka Mahenge, Morogoro kama si rais Kikwete kutaka uchunguzi ufanyike basi watu wangeendelea kuamini porojo za polisi kuwa walikuwa majambazi kumbe ni uongo.
Kwa muda nlioishi tz na tabia yangu ya kufuatilia mambo,si tukio la wafanyabiashara wa madini tu lililofanywa na polisi
 
Kwa muda nlioishi tz na tabia yangu ya kufuatilia mambo,si tukio la wafanyabiashara wa madini tu lililofanywa na polisi
Kisheria polisi haruhusiwi kuua mtu yeyote hata awe jambazi. Ni kosa la jinai na ndio maana baada ya kuua lazima watunge uongo kuonesha kwamba watuhumiwa walikaidi kujisalimisha na kuanza kupambana na polisi. Huo ni uongo wa kuwahadaa watu waone kuwa hakukuwa na namna ya kuwakamata na kuwafikisha mahakamani kama sheria inavyotaka.
 
Acha ujuaji,uporaji tu mipango na majambazi
 
Taarifa za polisi si za kuamini bila kuhoji. Mwaka 2006 polisi waliwaua wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, Morogoro na dereva taxi na kutangaza kuwa walikuwa ni majambazi. Ndugu wa wafanyabiashara hao wakakataa kuwa ndugu zao hawakuwa majambazi na wakamuomba rais Kikwete afutilie sakata hilo. Baada ya rais kuunda tume ndipo ikabainika kuwa watu wale hawakuwa majambazi.
Nakubaliana na hoja yako 100%
Mimi pia ni muumini wa utawala wa sheria.
Hata hivyo unataka kusema kuwa hili la polisi kuokoa watoto waliotekwa tusiliamini kwa kuwa hawaaminiki?
 
Nakubaliana na hoja yako 100%
Mimi pia ni muumini wa utawala wa sheria.
Hata hivyo unataka kusema kuwa hili la polisi kuokoa watoto waliotekwa tusiliamini kwa kuwa hawaaminiki?
Suala la kuokoa watoto waliotekwa na kuuawa kwa watuhumiwa ni mambo mawili tofauti. Uhai sio kitu cha kuchezea. Ikija kubainika kwamba haikuwa kweli nani atawarudishia uhai wao? Rejea sakata la wafanyabiashara wa madini wa mkoani Morogoro na yule dogo muuza madini aliyeuawa na polisi mkoani mtwara mwaka 2023 huku polisi wakisema ni mwizi wa pikipiki na baadae ikabainika ni uongo.
 
Kisheria polisi haruhusiwi kuua mtu yeyote hata awe jambazi. Ni kosa la jinai na ndio maana baada ya kuua lazima watunge uongo kuonesha kwamba watuhumiwa walikaidi kujisalimisha na kuanza kupambana na polisi. Huo ni uongo wa kuwahadaa watu waone kuwa hakukuwa na namna ya kuwakamata na kuwafikisha mahakamani kama sheria inavyotaka.
Ushawahi kukutana na jamabazi sugu ....anafanya uhalifu anafungwa miaka 30 anakaa miezi 2 jela anatoka na anaendelea na uhalifu
Hata nchi kama marekani nk wale wahalifu sugu huwa wanamalizana naoo maana hakuna namna

Ova
 
Suala la kuokoa watoto waliotekwa na kuuawa kwa watuhumiwa ni mambo mawili tofauti. Uhai sio kitu cha kuchezea. Ikija kubainika kwamba haikuwa kweli nani atawarudishia uhai wao? Rejea sakata la wafanyabiashara wa madini wa mkoani Morogoro na yule dogo muuza madini aliyeuawa na polisi mkoani mtwara mwaka 2023 huku polisi wakisema ni mwizi wa pikipiki na baadae ikabainika ni uongo.
Siku ukikutana nao waulize hivyo au ongea nao hivyo!
 
Taarifa za polisi si za kuamini bila kuhoji. Mwaka 2006 polisi waliwaua wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, Morogoro na dereva taxi na kutangaza kuwa walikuwa ni majambazi. Ndugu wa wafanyabiashara hao wakakataa kuwa ndugu zao hawakuwa majambazi na wakamuomba rais Kikwete afutilie sakata hilo. Baada ya rais kuunda tume ndipo ikabainika kuwa watu wale hawakuwa majambazi na hawakuwa na shtaka lolote la kihalifu.
Polisi nao ni binadamu kama sisi sote,kuna wanaofanya kazi kwa weredi wao na wapo wanaofanya kazi wakisukumwa na tamaa zao binafsi. Rejea hiyo sakata la wafanya biashara ya madini kutoka mahenge, Polisi tena wenye vyeo vya juu tu waliingiwa na tamaa na kuamua na kufanya walichofanya. Pia Miaka michache iliyopita arusha lilishawahi kutokea tukio kama hilo la mwanza la watoto kutekwa na watekaji kudai fidia, bahati mbaya ni kwamba baadhi ya watoto walipoteza maisha ila kijana aliyefanya ujinga huo ilikuja kujulikana kuwa alikuwa ni mdogo wa asikali wa FFU hapo arusha na alikuja naye kupigwa shaba kanda ya ziwa alikokuwa ameenda kujificha. 😎
 
Back
Top Bottom