Mwanza: Watu 6 wafariki kwa kugongwa na gari wakifanya mazoezi

Siyo powa alooh nimeacha rasmi achakitambi kije
 
Ruuh mimi na masela tunapasha kila siku road ya malimbe kuanzia Jeshini mpaka Saut chuoni ipo siku yetu tu gari litapita na sisi kmk tuuliwe kwasababu ile road walevi ni wengi

Hasa mimi naekimbiaga kama kichaa ipo siku gari litanivunja miguu kama sio kuniua...kuacha ndo siwezi
 
Hiyo barabara ya 77 kwenda Buswelu ni mpya na imejengwa vizuri sana kiasi cha kumvutia dereva kwenda mwendo wa speed , changamoto ya hiyo barabara ni nyembamba na ina kingo pande zote hapana pa kuchepukia, mwenyewe nimewahi kukosakosa mtu hapo Kiseke na kibaiskeli chake
 
Ni wakati sasa serikali irusishe maeneo ya wazi miji iwe na city parks watu wawe wanaenda kufanya mazoezi huko pia barabara ziongezwe kuweka nafasi ya wakimbia kwa miguu na waendesha baiskeri.
Inarudisha kutoka wapi wakati wameruhusu wavamizi?
 
Leseni yake ifungiwe, huu ni uzembe wa hali ya juu sana.
... Uchunguzi wa kina ufanywe kujua chanzo cha ajali na sio blah blah zilizotolewa eti "mwendokasi" kana kwamba kuna mtu alikuwa anapima speed aliyokuwa akiendeshea. Hakuna mtu anayeamka asubuhi nyumbani kwake kwenda kuua watu barabarani; never!
 
Kuna MTU alishaandika humu kua ni harari kufanya mazoezi kando ya high way
... sio tu hatari kufanya mazoezi barabarani; bali pia barabarani sio sehemu ya kufanyia mazoezi! Mbele ya macho ya sheria wote hao wana makosa kwa kuhatarisha usalama wa vyombo vya moto na watumiaji wengine wa barabara kisheria. Mark my words; by saa nne asubuhi kesi itakuwa imetupiliwa mbali na mahakama.
 
Pole Sana kwa wafiwa.
Haijapita hata mwezi mmoja tangu mwamba mmoja atuonye hapa jamii forum , kuhusu hatari za kufanya mazoezi barabarani.
Watanzania tuwe tunatii tunapoonywa, hatujui kuwa Mungu huzungumza na watu kupitia watu??
 
... Uchunguzi wa kina ufanywe kujua chanzo cha ajali na sio blah blah zilizotolewa eti "mwendokasi" kana kwamba kuna mtu alikuwa anapima speed aliyokuwa akiendeshea. Hakuna mtu anayeamka asubuhi nyumbani kwake kwenda kuua watu barabarani; never!
Usiseme NEVER. Kuna kitu kinaitwa
"Changamoto ya afya ya akili"
 
Ajali haina kinga. R.I.P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…