Mwanza: Watu 6 wafariki kwa kugongwa na gari wakifanya mazoezi

Mwanza: Watu 6 wafariki kwa kugongwa na gari wakifanya mazoezi

Nilisema na nitaendelea kusema👇👇👇

 
Watu 6 wamefariki dunia na wengine 14 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari binafsi, ambalo limewagonga wananchi waliokuwa wakifanya mazoezi kandokando ya barabara eneo la Sabasaba Ilemela Mwanza leo Julai 22, 2023 majira ya asubuhi.


=====
Taarifa za awali ni kwamba Watu 6 wamefariki dunia na wengine 14 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari binafsi, ambalo limewagonga wananchi waliokuwa wakifanya mazoezi kandokando ya barabara eneo la Sabasaba Ilemela, Jijini Mwanza.

Chanzo cha ajali ni mwendokasi na Dereva kutozungatia Sheria na alama za barabarani.

Miili ya Waliofariki na Majeruhi wa ajali wamepelewa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou toure.

============

UPDATES...
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Gideon Msuya “Imetokea katika Wilaya ya Ilemela, gari aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili T476 DZL ikitoka Sabasaba kuelekea Buswelu ilipoteza mwelekeo kutokana na mwendokasi na kusababisha ajali iliyoua watu 6, kujeruhi 14 waliokuwa wakifanya mazoezi ya kukimbia ambapo jumla yao walikuwa 27.

"Majeruhi wanne wapo Hospitali ya Bugando, wengine 10 wapo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sekou Toure.

“Juhudi za kumtafuta Dereva zinaendelea kwa kuwa alikimbia mara baada ya tukio hilo.”



6 people down, walikuwa wanategeneza afya zao, ila wamekufa kwa ajali, tena asubuhi....

Jamaa aliyewagonga atakuwa huru, ila ataishi maisha ya majuto sana sana kwa kweli...

Tukumbuke kusali wakati tunaendesha haya magari na kuwa makini, na mbali na simu.
 
Nina ndugu yangu anafanya mazoezi na rafiki zake nilimshaurigi zaidi ya mara mbili asiwe anakimbia (jogging) kwenye barabara au makazi ya watu angalau upate kiwanja mbona unafanya vizuri tu.

Sababu ya kumshauri kulishatokea tukio maeneo ya G5 mtu alikua anafanya tizi la mbio jioni katoka ufukweni zikapigwa kelele za mwizi mwamba hakupona.
Pili barabarani ndio kama hivyo mtu anaweza poteza uthibiti wa gari na mambo yakawa mengine.

Tujijali kila muda yuthamini kidogo haya maisha tuliopewa.
Pia unapokimbia barabarani kwa kupishana na magari ile hewa ya moshi wa magari si nzuri
 
Halafu unakuta msululu wa watu kwa kuigana kila mmoja anakimbia tu
Wapige marufuku tu
Mwenye akili timamu hawezi kufanya mazoezi barabarani
Taifa lililojaa wavivu, wazembe na walevi lazima lipinge mazoezi, watembea kwa miguu kila siku wanagongwa hamsemi marufuku itolewe watu kutembea barabarani, chanzo ni mwendo kasi wa dereva na lazima ulevi wa dereva. Wasikimbie barabarani watu elfu moja wakimbie kilometa 10 uwanjani inaingia akilini!!!viwanja vyenyewe viko wapi hata ingewezekana.
 
Ruuh mimi na masela tunapasha kila siku road ya malimbe kuanzia Jeshini mpaka Saut chuoni ipo siku yetu tu gari litapita na sisi kmk tuuliwe kwasababu ile road walevi ni wengi

Hasa mimi naekimbiaga kama kichaa ipo siku gari litanivunja miguu kama sio kuniua...kuacha ndo siwezi
Hua tunakaa tunawaangalia tu. Hasahasa nyie mnaokimbia kabla mwanga haujatoka.
Bora wale wajeda wanaokimbia asubuh na kuvaa nguo nyeupe.
Sasa hv beach za malimbe na luchelele zimepoa, lakn kipindi kile tamari, Jembe ni jembe, wag hill n.k ziko moto, mbona wengi tu walikua wanapigwa tairi.
Kaeni chonjo. Na hii barabarani nyembamba haitoshi.
 
Comment nyingi za watu humu zimenisikitisha sana.
Yaani watu wasifanye jogging
Vipi wale wanaotrain for marathons, long runs zao wafanye wapi especially sehemu za mijini.

Atleast;
Wanaofanya mazoezi wakimbie direction ya kuface magari
Wakimbie pembezoni mwa barabara sehemu za pedestrians
Kama Jogging ya group wawe na kibendera wa mbele ya group na nyuma ya group kuhakikisha usalama.

All in all, ajali haina kinga.
 
Mimi ni mkimbiaji.
Kwa kweli barabara huvutia na huhamasisha sana kukimbia, lakini ni hatari sana.

tatizo lipo kwa wakimbiaji.

1. Hawachagui barabara ambazo hazina traffic. Wao yoyote huingia.
huwa sielewi wanaokimbia mjini kabisa huwa wanapendezewa na nini, sababu huna amani wa uhuru.

2. Wanakimbia kundi, halafu unakuta wametanda barabara nzima. Kama wanamuongozaji unakuta yupo karibu na wakimbiaji, ilihari alipaswa kuwa mbele walau mita 100 akisafisha njia. Ukimbiaji wa kundi, ikitokea dharura, mobility ni ngumu sana.

mimi huwa sikimbii kundi kamwe, na hutumia barabara za nje ya mji zilizo wazi, vinginevyo ni uwanjani tu.

majeruhi, wapone haraka.
 
Hua tunakaa tunawaangalia tu. Hasahasa nyie mnaokimbia kabla mwanga haujatoka.
Bora wale wajeda wanaokimbia asubuh na kuvaa nguo nyeupe.
Sasa hv beach za malimbe na luchelele zimepoa, lakn kipindi kile tamari, Jembe ni jembe, wag hill n.k ziko moto, mbona wengi tu walikua wanapigwa tairi.
Kaeni chonjo. Na hii barabarani nyembamba haitoshi.
dah, umenikumbusha mbali sana ulivyotaja Hizo beach.

siku hizi hazifanyi kazi?
 
Ruuh mimi na masela tunapasha kila siku road ya malimbe kuanzia Jeshini mpaka Saut chuoni ipo siku yetu tu gari litapita na sisi kmk tuuliwe kwasababu ile road walevi ni wengi

Hasa mimi naekimbiaga kama kichaa ipo siku gari litanivunja miguu kama sio kuniua...kuacha ndo siwezi
Mdomo unaumba
 
Ambacho ningependa kujua,hao wanapata ajali za kugongwa barabarani wanakuwa barabarani kabisa au pembezoni,maana kwenye barabara zetu baada ya lami pembeni kuna ukingo wa mchanga,kwanini wasikimbie huko pembeni au huko pembeni ndiko gari zinawafuata....?
 
Back
Top Bottom