Mwanza: Watu 6 wafariki kwa kugongwa na gari wakifanya mazoezi

Mwanza: Watu 6 wafariki kwa kugongwa na gari wakifanya mazoezi

Nina ndugu yangu anafanya mazoezi na rafiki zake nilimshaurigi zaidi ya mara mbili asiwe anakimbia (jogging) kwenye barabara au makazi ya watu angalau upate kiwanja mbona unafanya vizuri tu.

Sababu ya kumshauri kulishatokea tukio maeneo ya G5 mtu alikua anafanya tizi la mbio jioni katoka ufukweni zikapigwa kelele za mwizi mwamba hakupona.
Pili barabarani ndio kama hivyo mtu anaweza poteza uthibiti wa gari na mambo yakawa mengine.

Tujijali kila muda yuthamini kidogo haya maisha tuliopewa.
Arusha kuna jamaa huwa anakimbia kinyumenyume kwenye barabara kuu,ujinga
 
Comment nyingi za watu humu zimenisikitisha sana.
Yaani watu wasifanye jogging
Vipi wale wanaotrain for marathons, long runs zao wafanye wapi especially sehemu za mijini.

Atleast;
Wanaofanya mazoezi wakimbie direction ya kuface magari
Wakimbie pembezoni mwa barabara sehemu za pedestrians
Kama Jogging ya group wawe na kibendera wa mbele ya group na nyuma ya group kuhakikisha usalama.

All in all, ajali haina kinga.
Wajinga nyie
 
Huna hoja. Kukimbia kando ya barabara ni sawia na kutembea kando ya barabara. Ni kwa sababu Tanzania ni taifa la watu wapuuzaji na wajinga. Hakuna madereva bali waendesha vyombo vya moto. Usiniulize tofauti. Chukua hatua.
Mhaya umekasirika sana.

Miundombinu ya Tanzania hairuhusu magari na watu kukimbia kwa pamoja.

Nchi za wenzetu wana sehemu za mazoezi
 
Na ile njia ilivyo finyu!

Pale SAUT viwanja vingi mno kuanzia Nsumba, Nganza, malimbe vipo vingi, hata hapo mwanzo nyegezi kona ukiwa unashuka kuna kiwanja kizuri tu mkono wa kulia. Better mjichimbie uwanjani kuliko kile kipisi cha barabara, kama vipi andikeni wosia kabisa.
Mtawaonaje wanakimbia kama wakijifungia kiwanjani?
 
Yote yatasemwa ila kosa litakuwa palepale Kuna madreva wengi sana Tanzania wasiojali sheria Wala utu wamejaa hasira na kisirani wenye haraka zisizo na maana
Sawa hao wanajogi wamegongwa kwa hiyo wangekuwa wanatembea ama wamekaa wanangoja usafiri ndio dreva asingewagonga tena wanajogi mi nadhani ni rahisi kuwaona na kurekebisha mwendo ndivyo tunavyofundishwa driving school
Wote tunajua hatuna barabara rafiki kwa hiyo lazima kulindana barabarani
 
Mtawaonaje wanakimbia kama wakijifungia kiwanjani?
Shida inaanzia hapo. Kwa wengi ulimbukeni ndo unawasumbua.

Huwa nashangaa vyuoni kuna viwanja vingi ila wanachuo utakuta wamekomaa barabarani tu! Huu ujinga kuna madogo kutoka vijijini ndani huko walinishirikisha first year nikawakata bango, tangu siku hiyo sijawaona tena wakiingia barabarani, nadhani watakuwa wanafanya hivyo wakienda makwao huko.
 
Shida inaanzia hapo. Kwa wengi ulimbukeni ndo unawasumbua.

Huwa nashangaa vyuoni kuna viwanja vingi ila wanachuo utakuta wamekomaa barabarani tu! Huu ujinga kuna madogo kutoka vijijini ndani huko walinishirikisha first year nikawakata bango, tangu siku hiyo sijawaona tena wakiingia barabarani, nadhani watakuwa wanafanya hivyo wakienda makwao huko.
Kwanza ni kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara

Ni kuhatarisha maisha yao na ya wengine, maana wanakimbia upande wa barabara wote
 
Mhaya umekasirika sana.

Miundombinu ya Tanzania hairuhusu magari na watu kukimbia kwa pamoja.

Nchi za wenzetu wana sehemu za mazoezi
Miundombinu yetu ni hovyo.

Ni kweli usemavyo. Hapa kwetu si kukimbia tu hata kutembea kando ya barabara ni hatari tupu ukijumlisha na ujinga wa watu wetu ni balaa juu ya balaa.
 
Kuna siku moja nikiwa natembea traffic akaniita akaniambia nisitembee huku nikiwa nimeyapa magari mgongo nitembee nikiwa nayaona kwa mbele yanavyokuja nikaweka hilo kichwani hadi leo nikitoka matembezi na shangazi yenu [emoji23][emoji23][emoji3] kanuni ni hiyo
 
Ukisoma humu unagundua namna watu hawafahamu sheria za barabara na mambo yake.
Miundombinu yetu ni hovyo ukijumlisha na kuwa na wajingawajinga waendesha vyombo vya moto inawaweka watu wengine katika hatari pindi wanapotembea/kukimbia kando ya barabara.
 
Barabara za mtaani hakuna?
Ruuh mimi na masela tunapasha kila siku road ya malimbe kuanzia Jeshini mpaka Saut chuoni ipo siku yetu tu gari litapita na sisi kmk tuuliwe kwasababu ile road walevi ni wengi

Hasa mimi naekimbiaga kama kichaa ipo siku gari litanivunja miguu kama sio kuniua...kuacha ndo siwezi
 
Hao wanaokimbiaga pembeni mwa barabara jogging huwa nawashanga
Barabara zetu zenyewe sehemu kubwa hayana mazingira salama kwa watembea kwa miguu/jogging

Ova
 
Kuna siku moja nikiwa natembea traffic akaniita akaniambia nisitembee huku nikiwa nimeyapa magari mgongo nitembee nikiwa nayaona kwa mbele yanavyokuja nikaweka hilo kichwani hadi leo nikitoka matembezi na shangazi yenu [emoji23][emoji23][emoji3] kanuni ni hiyo
Kweli kabisa, mimi niliwahi kufikiria nikaona haiji kabisa kuyapa mgongo magari, nikachagua kutembelea upande wa kulia mara zote niwapo barabarani. Kumbe hata trafiki wanaelekeza hivyo!
 
Ajali zinatokea kila siku
Wenye mabasi kila kukicha wanaua na hakuna anaehukumiwa kifo

Sehemu za mazoezi zitengwe na sio barabarani
Sehemu za wazi zote zimeuzwa na washenzi wenye tamaa
Mpaka viwanja vya shule vimeuzwa

Zamani mpaka makahama zilikuwa na maeneno makubwa sana mpaka mpira tulikuwa tunacheza jioni

Police walikuwa na maeneo makubwa
Ila kila mahali wameuza watu wenye tamaa
Hao ndio wa kunyongwa sasa
Usiwasahau wa bandari nao!
 
Watu 6 wamefariki dunia na wengine 14 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari binafsi, ambalo limewagonga wananchi waliokuwa wakifanya mazoezi kandokando ya barabara eneo la Sabasaba Ilemela Mwanza leo Julai 22, 2023 majira ya asubuhi.


=====
Taarifa za awali ni kwamba Watu 6 wamefariki dunia na wengine 14 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari binafsi, ambalo limewagonga wananchi waliokuwa wakifanya mazoezi kandokando ya barabara eneo la Sabasaba Ilemela, Jijini Mwanza.

Chanzo cha ajali ni mwendokasi na Dereva kutozungatia Sheria na alama za barabarani.

Miili ya Waliofariki na Majeruhi wa ajali wamepelewa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou toure.

============

UPDATES...
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Gideon Msuya “Imetokea katika Wilaya ya Ilemela, gari aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili T476 DZL ikitoka Sabasaba kuelekea Buswelu ilipoteza mwelekeo kutokana na mwendokasi na kusababisha ajali iliyoua watu 6, kujeruhi 14 waliokuwa wakifanya mazoezi ya kukimbia ambapo jumla yao walikuwa 27.

"Majeruhi wanne wapo Hospitali ya Bugando, wengine 10 wapo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sekou Toure.

“Juhudi za kumtafuta Dereva zinaendelea kwa kuwa alikimbia mara baada ya tukio hilo.”

UPDATES
======

Mwanza. Watu sita wamefariki papo hapo na wengine 16 wakijeruhiwa baada ya kugongwa na gari aina ya Hilux double cabin eneo la Shule ya Msingi Lumala Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Gideon Msuya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo asubuhi ya leo Julai 22, 2023 wakati kikundi cha vijana kilichotambulika kwa jina la Adden hotel kikiwa kinafanya mazoezi ya kukimbia katika barabara ya sabasaba kuelekea Kiseke wilayani humo.

Msuya amesema msako wa dereva wa gari hiyo unaendelea baada ya kulitelekeza kwenye kituo cha mafuta kisha yeye kutokomea kusikojulika.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sekouture, Dk Bahati Msaki amesema wamepokea miili ya watu watano huku mmoja akifariki akipatiwa matibabu hospitalini hapo na majeruhi 8 wanaendelea na matibabu huku 8 wakipatiwa rufaa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa uangalizi maalum.

“Vijana hao walikuwa wanafanya mazoezi ya mwendo wa pole wakiwa na kundi lao Linalotambulika kwa jina la Adden hotel,”amesema Dk Msaki

Dk Msaki amesema miili ya marehemu ipo katika Hospitali ya Mkoa Sekou Toure huku taratibu za kuikabidhi kwa ndugu zinaendelea kuratibiwa na hospital ya Sekou Toure na Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza.

“Nitoe pole kwa familia waliopoteza wapendwa wao na tuendelee kuwaweka kwenye maombi majeruhi wote wapate uponyaji wa haraka na waruhusiwe warudi nyumbani kuendelea na majukukumu yao,”amesema Dk Masala
View attachment 2696406View attachment 2696408
Kwani gari sio lake huyo dereva?
 
Back
Top Bottom