Mwanza: Watu 6 wafariki kwa kugongwa na gari wakifanya mazoezi

Mwanza: Watu 6 wafariki kwa kugongwa na gari wakifanya mazoezi

Fanya mazoezi walisema, ili uishi maisha mingi walisema.

Dunia hii.
Wapumzike kwa amani.
 
Pole sana kwa wafiwa na majeruhi. Tunawaombea Mungu awapumzishe mahali pema marehemu wote na pia awaponye majeruhi.
Mbona kama daktari anatoa taarifa nyingi ambazo hata hazimhusu? Amejuaje jina la kikundi na taarifa nyingine? Yeye abaki upande WA medicals tu
 
Kuna watu wanatembea na earphone na earpods hao kujeruhiwa ni nukta
Huyo nimimi kabisa mkuu mi bila earphone cwez kimbia ila nikiwa na phone nakichafua toka kijitonyama mlimani city, mwenge kawe kurudi mpaka moroco mzuka ukiwa mwingi mpaka posta nafika
 
Ajali zinatokea kila siku
Wenye mabasi kila kukicha wanaua na hakuna anaehukumiwa kifo

Sehemu za mazoezi zitengwe na sio barabarani
Sehemu za wazi zote zimeuzwa na washenzi wenye tamaa
Mpaka viwanja vya shule vimeuzwa

Zamani mpaka makahama zilikuwa na maeneno makubwa sana mpaka mpira tulikuwa tunacheza jioni

Police walikuwa na maeneo makubwa
Ila kila mahali wameuza watu wenye tamaa
Hao ndio wa kunyongwa sasa
Nimesikitika sana eneo la wazi la Kitaa ambalo tulikulia tunacheza mpira likijulikana masoko yaani kiongozi wa ngazi ya juu Kabisa ya chama na serikali kajenga bungallow ndani ya miezi3. Sipingi maendeleo binafsi ya mtu ila why now? Tena pahala pa open space ya kusenga soko? au kwa kuwa ni ushuani sijui, hajaona pahala pengine? yaani tunaowategemea watulinde na kuktututea wanyonge ndio wana wanatupurua.
 
Kwa kweli inakera sana halafu kuna wanasheria ambao kazi yao kutetea wanasiasa badala ya Umma

Inauma sana
Wengine tumeshuhudia mpaka ardhi za misikiti, maeneo ya wazi yakigawanywa na wenye tamaa huku wengi waliouza wamekufa kwa thamani ndogo
 
Halafu unakuta msululu wa watu kwa kuigana kila mmoja anakimbia tu
Wapige marufuku tu
Mwenye akili timamu hawezi kufanya mazoezi barabarani
Kwa Tanzania siyo kufanya mazoezi tu ila hata kutembea kando kando ya barabara ni hatari. Mimi nikiwa Dar huwa natembea kwa wasiwasi mno ninapokuwa kwa miguu kwani barabara nyingi hazina sehemu rasmi ya waenda kwa miguu au kama zipo, huwezi kujua barabara ni ipi na sehemu ya waenda kwa miguu ni ipi. Magari nayo yanaenda mwendo wa hatari kweli kweli. Kuhusu hii ajali, ni matokeo mengine ya jinsi sisi raia tunavyolipa gharama kubwa kwa sababu ya kukaa kimya pale viongozi wetu wanapofanya uzembe. Kuna uzembe mkubwa sana kwenye utengenezaji wa barabara kwani hazikidhi viwango. Waliofariki au kuumia ni victims tu wa uzembe wa serikali.
 
Rest in peace Amani, tumekupumzisha leo kwenye nyumba yako ya milele!
 
Kwa Tanzania siyo kufanya mazoezi tu ila hata kutembea kando kando ya barabara ni hatari. Mimi nikiwa Dar huwa natembea kwa wasiwasi mno ninapokuwa kwa miguu kwani barabara nyingi hazina sehemu rasmi ya waenda kwa miguu au kama zipo, huwezi kujua barabara ni ipi na sehemu ya waenda kwa miguu ni ipi. Magari nayo yanaenda mwendo wa hatari kweli kweli. Kuhusu hii ajali, ni matokeo mengine ya jinsi sisi raia tunavyolipa gharama kubwa kwa sababu ya kukaa kimya pale viongozi wetu wanapofanya uzembe. Kuna uzembe mkubwa sana kwenye utengenezaji wa barabara kwani hazikidhi viwango. Waliofariki au kuumia ni victims tu wa uzembe wa serikali.
Sisi hatuna kitu cha kujivunia hata kimoja katika hii dunia. Utasikia tunajivunia amani uchwara. Amani ya mazindiko na nguvu ya dola.
 
Maisha buana yaache tu unajaribu kufanya mazoezi kujiweka fiti shetani anakusomba hukohuko wanakufukia na afya yako
 
Ukute kati ya hao marehemu kuna mwamba alikuwa anatoka na wife wa dereva aliyegonga hao jamaa waliokuwa wanafanya mazoezi.
Jamaa mwenye mke akawaza akaona isiweshida wanapofanyia mazoezi si nina pafahamu ngoja nimfyekelee mbali then itafahamika as traffic case, na hivi gari ina bima kubwa case itakuwa closed kwa faini tu.
Done 🏃‍♂️🏃‍♂️🤔
 
Mwanadamu aliezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi nazo hujaa taabu(Ayubu1:4)

Raha ya milele uwape ee Bwana na mwanga wa milele uwaangazie wapumzike kwa amani🙏🏻
 
Back
Top Bottom