Taarifa ya awali ya jeshi la polisi kuhusu kushambuliwa kwa padri kitima ina viashiria vyote vya kumchafua na kuchafua taswira ya kanisa katoliki.
- Wanadai alikuwa katika kantini akipata vinywaji (Wakiwa na maana akilewa na kuwayawaya) HAKUNA SEHEMU WAMETAJA KWAMBA Alishambuliwa akiwa katika makazi yake wametaja Kantini bar strategically ili kufikisha ujumbe kwamba kuna ulevi ndani ya kanisa.
- Wakaenda mbali zaidi kwamba kulikuwa na ugomvi wa walevi wawili ili baadae kupenyeza ajenda kuwa ulikuwa ugomvi wa kawaida unaochangiwa na walevi kungombea mambo mbalimbali kama mapenzi n.k report ya awali haijaeleza kabisa huyo mtuhumiwa aliingiaje katika makazi ya kanisa, je ni mmoja ya wahusika ndani ya kanisa hilo, je kwenye orodha ya wageni au daftali la walinzi aliingia kama mgeni au mlevi taarifa inasema tu mtuhumiwa ni mkazi wa kurasini pasipo kutaja kurasini hapo baraza la maasikofu au kurasini kota za polisi,
- Eneo aliposhambulowa; Hili nalo linaibua maswali mengine, Kwamba walevi wenzake walimfuata maliwatoni kumshambulia au alijibamiza mwenyewe ukutani kwa kuwayawaya na ulevi wa pombe. Repoti haizungumzii kabisa makazi yake ..yaani kwa lugha nyingine ni sawa na mtu ashambuliwe nyumbani kwake halafu wasiseme alishambuliwa katika makazi yake bali alikuwa sebuleni anakunywa maji.
- Taarifa imetolewa haraka sana pasipo kuonesha mtuhumiwa baada ya shambulio alibakia hapo kupata vinywaji au alijisalimisha polisi au ndo yule aliyemtishia kitima mtandaoni kuwa atamshambulia au ni mwingine?
- Taarifa ya madakitali inasemaje, je walipokea mlevi mmoja mwenye jina kitima?
- Vitabu vya walinzi na walinzi je wanataarifa za ugeni wa mgeni tajwa hapo barazani?