Mwauwasa sisi ni binadamu sio ngamia

Mwauwasa sisi ni binadamu sio ngamia

Hamissi Hamza Jr

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2020
Posts
561
Reaction score
1,149
Inasikitisha Sana kwa Ukanda Wa Pembezoni Mwa Ziwa Viktoria Kuwa na Tatizo sugu La Huduma ya Maji,

Mkoa Wa Mwanza Imekua Si Changamoto tena imekua Kama ni Wajibu wa Wananchi Kukosa Huduma Hii Muhimu Kwa Wiki kadhaa au Miezi,Bahati Mbaya Hakuna Taarifa zinazotolewa Wazi kwa Umma Kama kutakua na ukosefu wa Huduma Na Bahati Mbaya Zaidi Hamna Uwajibikaji wa Moja Kwa Moja Kwa Watendaji Na Wizara Husika.

JE???

1.Je Mapato Ni madogo Kuliko Gharama Za Uendeshaji?

2.Je Maji Ziwa Victoria yameisha Mnayafata Bahari ya Hindi au Saivi ni Ya kuchimba?

3.Je Imewachosha tu kazi mnaona Kuhudumia jamii kwa wito Ni mzigo?


Miaka 65 Ya Uhuru Ni Aibu Isiyo Himilivu kuendelea Kulalamikia Maji Jifunzeni Uwajibikaji kama Haiwezekani Binafsisheni kwa Taasisi Binafsi Wananchi Tupate Huduma za Uhakika,Sisi Ni Binadamu tunahitaji Maji kila Siku Sio Ngamia Kwamba Tunahitaji mala Moja kwa miezi.
 
Tanzania haikupaswa watu walalamike kukosa maji.
Kama sisi tumeshindwa basi waje mabeberu tuwape miradi ya kusambaza maji tuone kama kilio Cha ukosefu wa maji kitakuwepo
 
Back
Top Bottom