Diamond sio mmiliki mkuu wa makampuni kama wasafi tv, wasafi radio, wasafi bet, Diamond karanga (r.i.p), yeye nafasi yake huwa ni co-owner, anachofanya ni kuwekeza tu jina lake na kuchukua asilimia zake kwenye faida. Uhakika wa 40%-49% ya umiliki na faida upo chini yake kwa kutoa tu jina wasafi litumike kwenye kampuni.
Hata Azam Bakhresa nae hufanya hivyo Kwa baadhi ya makampuni yanayotambulika kwa Brand yake maarufu ya Azam, wawekezaji wanaweza kuwa huko nchi nyingine, wao wanamuomba Bakhresa awaruhusu watumie jina la Azam kwa makubaliano ya mgao kwenye umiliki, faida, meejment, n.k
Kpindi kile Diamond Karanga, wahindi walipoona zinauzika sana walitaka kuleta janja janja na ulafi baada ya kuona biashara inalipa, wakaanza kulalamika kwamba wananyonywa kwasababu Diamond kachangia tu jina na anapata mgao mkubwa wakati hajachangia mtaji, Leo hii hizo karanga zipo wapi? Nadhani mmeiona thamani ya jina hapo.
Na hivi ndivyo hali ilivyo kwenye Wasafi tv na Wasafi fm, Kusaga ndie alieweka mpunga kununua vifaa vingi lakini Diamond alichangia tu jina kwa maelewano kwamba atamiliki hisa zinazompa significant influence.
Hata hii kampuni yake mpya ya kubet ya Wasafi bet, ni makubaliano baina ya kampuni ya kubeti ya nchini Kenya inayoitwa odibet, ni kampuni ambayo ingeingia hapa nchini ingepata wakati mgumu sana kupata jina na wateje, kwa hiyo wameamua kutumia shortcut kwa kutumia jina la Wasafi kwa makubaliano kwamba faida wagawane kwa asilimia ambazo ni si haba.
Kama unaona huu ni unyonyaji, hii ni nchi huru, mlango upo wazi unatafuta kwengine
Hongera sana Diamond