Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 153
- 161
MWEKEZAJI kwenye Shamba la VASSO lililopo kijiji cha Dakau wilaya ya Moshi vijijini, Fons Nijenhuis(73) raia wa Uholanzi, amedai kufukuzwa kwenye shamba hilo na watu wasiojulikana huku kundi kubwa la watu likivamia makazi yake na kufanya uharibifu mkubwa wa mali pamoja na kufanya uporaji wa mali na pesa.
Mbali na uharibifu huo wa mali, watu hao pia wanadaiwa kuua farasi wake wawili pamoja na kupora fedha kiasi cha Euro elfu kumi huku akidai kuumizwa vibaya mke wake na kuiomba serikali iingilie kati kumrejesha shambani akida kuondolewa kwake hakujafuata taratibu za kisheria ikiwamo kutokupewa hati ya kusudio la kuondolewa shambani hapo.
Fons aliyeingia nchini Tanzania mwaka 1982 akitokea nchini Zambia, aliingia mkataba wa kuwekeza kwenye shamba hilo mwaka 2003 kwa mkataba wa miaka 30 na chama cha ushirika wa mazao cha Kilbosho kati kabla ya kuhuisha mkataba huo mwaka 2021 na kuurefusha hadi mwaka 2058.
Fons ambaye ni mbia kwenye shamba hilo kwa aslimia 50 huku asilimia 50 zikimilikiwa na wabia wenzake Hans Baaet na Tjerk Scheflema amezungumza na waandishi wa habari mjini moshi na kudai kitendo alichofanyiwa hakipaswi kufanya kwenye nchi kama Tanzania.
"Wamenifukuza kama takataka, huu ni unyama na haya mambo yanafanyika Zimbabwe siyo Tanzania, naomba Rais Mama Samia Suluhu Hassan aingilie kati, mimi siondoki hapa mpaka wanirudishie shamba langu", alisikika Fons akilalamika.
Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro Kiseo Nzowa amezungumza na waaandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo na kudai anafuatilia na atalitolea Taarifa huku viongozi wa Chama cha Ushirika Kibosho kati nao wakizungumzia tukio hilo.
Mwenyekiti wa Chama hicho Fabian Mallya amesema chama hakihusiki na kufukuzwa kwa mwekezaji huyo kwenye shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 181.13.
Nini hatima ya mgogoro katika shambo hilo?,fuatilia hapa