Mwele, Lissu na Membe mmeonesha ujasiri. Kinana umeudhalilisha utu wako

Mwele, Lissu na Membe mmeonesha ujasiri. Kinana umeudhalilisha utu wako

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Dr. Mwele alijua yuko sahihi na wao walijua yuko sahihi ndio maana hadi leo hawaachi kumtaja.

Tundu Lissu alipigwa risasi zaidi ya 16 si kwa sababu alikuwa na kosa, bali kosa lake ni kuuzungumza ukweli, hajaomba radhi kwa kuwa alisema alichokuwa anakiamini.

Membe kasema yeye siyo mhalifu kwa nini aombe radhi? Kinana inawezekana umesamehewa na binadamu ila sidhani kama Mungu amekusamehe kwa vile umeudanganya moyo wako.

Tanzania tulikuwa na majasiri wachache wa aina hii waliowaambia watawala ukweli akiwepo, Gavana wa kwanza wa benki kuu Mtei, Kambona, Abdu Jumbe, Mch. Mtikila.

Wengi wa Watanzania tu waoga au wanafiki au hatujiamini au tunajali matumbo yetu na kuacha maslahi mapana ya nchi yetu kama akina Mwigulu, January, Nape, Mo, Lipumba, Mbatia, ambao kazi yao ni kusifu watawala walio madarakani.

Tenda wema ili kulisaidia taifa na siyo serikali ambazo zinapita na historia itakukumbuka.

Hongera Dr. Mwele, Lissu na Membe, mmeonyesha ujasiri wa kuigwa na vizazi vilivyopo na vijavyo. Mnastahili tuzo maalumu na taifa litawakumbuka.
 
Nafikiri kila mtu na uhuru wa kuchagua na kusimamia kile anachoona kinafaa tusiwabeze na kuwaona waoga wakati walisimamia walichoamini mkuu
#JikingeWakingeWengine
 
Sio msafi anaogopa kuswekwa ndani na dikteta
Nafikiri kwa utawala huu hata akiwa huko (CCM) bado kama mchafu atafichuliwa tu , hayo ya Udikteta pengine wa wivu wa pwani unakusumbua Mpwaa kama mpwaaa
 
Mbona unaweweseka na kuteseka Sababu ya uamuzi wa mwanaume.

Tulia acha watu hekima na busara itawale
 
nimemwelewa kinana

'if u cant fight them join them'

ni rahisi kumshinda adui ukiwa ndani
 
Huyo Dr. Mwale akumbukwe kwa lipi? na huyo Membe? sema wewe utawakumbuka siyo taifa hakuna na hatokuwepo mwenye mpango nao, hebu acha kwanza unafki mwenyewe, labla kidogo Lisu ni mwanaharaki siyo hao wengine ni kama kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa
 
Mbona ninashindwa kuunganisha Mo na hawa wengine?, hawa wote ni wanasiasa, Mo ameingiaji hapa, tafadhali dadavua kidogo.
 
Nafikiri kwa utawala huu hata akiwa huko (CCM) bado kama mchafu atafichuliwa tu , hayo ya Udikteta pengine wa wivu wa pwani unakusumbua Mpwaa kama mpwaaa
Ni nani msafi huko Ccm ?!
Nani !! Hata hao wanaojiona wazalendo ni zaidi ya wahalifu
 
Kuna wakati simlaumu sana Col. Kinana... Ana background iliyochafuka sana.... Asipopiga goti sasa anatambua wazi what will come next to him

Jr[emoji769]
 
huyo Dr. Mwale akumbukwe kwa lipi? na huyo Membe? sema wewe utawakumbuka siyo taifa hakuna na hatokuwepo mwenye mpango nao ,hebu acha kwanza unafki mwenyewe, labla kidogo lisu ni mwanaharaki siyo hao wengine ni kama kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa
Kila mmoja atakumbukwa kwa ujasiri wa kazi yake siyo lazima wote wawe wanasiasa.
 
Shida ipo pale pale mbona hata Chadema wanamlalamikia Mwenyekiti kufanya ufisadi na ufisidi wa kutosha Ngoma droo
Inategemea hizo lawama zinatolewa na nani na kwa mazingira gani, siyo mtu amepewa maneno ya kusema wewe bila kuchuja unayaamini.
 
Back
Top Bottom