Mwele, Lissu na Membe mmeonesha ujasiri. Kinana umeudhalilisha utu wako

Mwele, Lissu na Membe mmeonesha ujasiri. Kinana umeudhalilisha utu wako

Inategemea hizo lawama zinatolewa na nani na kwa mazingira gani, siyo mtu amepewa maneno ya kusema wewe bila kuchuja unayaamini.
tuwe na ngozi ngumu kama ya mamba ili hata tukikwaruzwa tusisikie maumivu kwa kuwa na sisi tuna kucha zinazowakwaruza wengine
 
Kila mmoja atakumbukwa kwa ujasiri wa kazi yake siyo lazima wote wawe wanasiasa.
ina manufaa gani kwa taifa, mfano unahisi Membe ni jasiri au amekosa alichokuwa anakitaka ameona atafute kwa njia nyingine?
 
tuwe na ngozi ngumu kama ya mamba ili hata tukikwaruzwa tusisikie maumivu kwa kuwa na sisi tuna kucha zinazowakwaruza wengine
Maneno yako ni mazuri kwa Rais asiyependa kukosolewa.
 
ina manufaa gani kwa taifa, mfano unahisi Membe ni jasiri au amekosa alichokuwa anakitaka ameona atafute kwa njia nyingine?
Kama kwako siyo jasiri kwa wengine jasiri, kwa rais wa awamu hii kumwambia sikuombi radhi inatakiwa kuwa na ujasiri wa kiasi fulani, labda ungekuwa utawala wa Kikwete sio huu.
 
Kama kwako siyo jasiri kwa wengine jasiri, kwa rais wa awamu hii kumwambia sikuombi radhi inatakiwa kuwa na ujasiri wa kiasi fulani, labda ungekuwa utawala wa Kikwete sio huu.
hapo ina mpa sifa gani ya kukumbukwa na taifa? si individual interest tu hizo hata ww unaweza
 
Yule aliyekwenda kupiga ramli akaambiwa atakayeitoa ccm madarakani ni Tindu lissu wakataka kumuua kabla utabiri haujatimia
 
Huo msamaha mbona sijasikia tamko lolote kwa mkulu kuwa kamsamehe wala sijaona barua ya Msigwa
 
Kweli mtu anapokamuliwa Jipu lazima tu atalalamika. Lakini ndio dawa. ZIKA waliithibiti vipi. Lisu nilimkubali lkn alipokuja na hoja ya MIGA basi sijapata kumuelewa tena.
 
Sijakuelewa ulicho kiandika labda sababu ya njaa yangu.

Kwa hiyo kwako mtu anae pingana na serikali ni shujaa, sio?
 
Mbona ninashindwa kuunganisha Mo na hawa wengine?, hawa wote ni wanasiasa, Mo ameingiaji hapa, tafadhali dadavua kidogo.
Nilicho muelewa mtoa Utopolo ni kwamba.
Yeyote atakae isifia serkali ama kuunga juhudi za mheshimiwa Rais, yeye anamtafasiri kama ni adui, hata akiwa baba yake mzazi.
 
Sijakuelewa ulicho kiandika lbd sababu ya njaa yangu.

Kwahiyo kwako mtu anae pingana na serkali ni shujaa, sio?
Kwanza unatakiwa ujue kapinga nini, kwani serikali haipingwi?
 
Ndio maana nikatanguliza, neno "sijakuelewa sababu ya njaa yangu".
Kwanza unatakiwa ujue kapinga nini, kwani serikali haipingwi?
Ngoja nitafute rizk ya mchana huu wenda nika muelewa.
 
Maskini Kinana, anayepaswa kuombwa msamaha ni Mungu sio binadamu aliye udongo na mavumbi
 
Kilichonishangaza yule alietakiwa kuombwa msamaha ndio alieomba msamaha
 
Kwa wote uliowataja.

Ungetembea na Mh. Lissu tu.

Mwalimu wa waliobaki anacheka tu vile wanafunzi wao wanavyotajwatajwa.
 
Nafikiri kila mtu na uhuru wa kuchagua na kusimamia kile anachoona kinafaa tusiwabeze na kuwaona waoga wakati walisimamia walichoamini halmashauri mkuu
#JikingeWakingeWengine
Huo umo ndani ya katiba kila mtu anastahili.
Lakini linapokuja suala la ukweli ni lazima usemwe
 
Mmeshanyooka miaka mitano tu bado mitano mingine vumilieni ndio dozi ya mwisho!
Mmebaki wachache sana mnaoshangilia hata kwenye msiba.
Huko kwenu wote mmenyooka tayari.

Mkwere kanyooka, chinga, ruksa je,!
Makamba na umbambala wake!
Kinana, nape.
Kama hawa manguli ndani ya ccm wamenyooshwa, ninyi vimburu mtaonekana wapi?
 
Sasa dr mwele nae kaonesha ujasiri gani sasa ? Kwani kile alichokifanya nacho kinastahili kuonekana ni jasiri ? Kwa ujasiri upi alioufanya au unataka kutuambia nn ?
 
Nafikiri kwa utawala huu hata akiwa huko (CCM) bado kama mchafu atafichuliwa tu , hayo ya Udikteta pengine wa wivu wa pwani unakusumbua Mpwaa kama mpwaaa
Kiluvya kumekupumbaza njoo mjini
 
Back
Top Bottom