Mwele, Lissu na Membe mmeonesha ujasiri. Kinana umeudhalilisha utu wako

Mwele, Lissu na Membe mmeonesha ujasiri. Kinana umeudhalilisha utu wako

Nimemhurumia sana Kinana , jini walilolifuga yeye na Kikwete lishatoka kwenye chupa linatafuna watoto
Noma sana hilo jini lina kisasi kama CHOTE kinana akidindiana naye anaweza KUTEMESHWA NDOANO ila JASUSI Mbobezi anamjua IN and OUT ndio maana kasema hawezi kuomba RADHi.
 
Dr. Mwele alijua yuko sahihi na wao walijua yuko sahihi ndio maana hadi leo hawaachi kumtaja.

Tundu Lissu alipigwa risasi zaidi ya 16 si kwa sababu alikuwa na kosa, bali kosa lake ni kuuzungumza ukweli, hajaomba radhi kwa kuwa alisema alichokuwa anakiamini.

Membe kasema yeye siyo mhalifu kwa nini aombe radhi? Kinana inawezekana umesamehewa na binadamu ila sidhani kama Mungu amekusamehe kwa vile umeudanganya moyo wako.

Tanzania tulikuwa na majasiri wachache wa aina hii waliowaambia watawala ukweli akiwepo, Gavana wa kwanza wa benki kuu Mtei, Kambona, Abdu Jumbe, Mch. Mtikila.

Wengi wa Watanzania tu waoga au wanafiki au hatujiamini au tunajali matumbo yetu na kuacha maslahi mapana ya nchi yetu kama akina Mwigulu, January, Nape, Mo, Lipumba, Mbatia, ambao kazi yao ni kusifu watawala walio madarakani.

Tenda wema ili kulisaidia taifa na siyo serikali ambazo zinapita na historia itakukumbuka.

Hongera Dr. Mwele, Lissu na Membe, mmeonyesha ujasiri wa kuigwa na vizazi vilivyopo na vijavyo. Mnastahili tuzo maalumu na taifa litawakumbuka.
Anaogopa kurudishwa Somalia
 
“Tenda wema ili kulisaidia taifa na siyo serikali ambazo zinapita na historia itakukumbuka”.

Rest In Peace Dr. Mwele.
 
Back
Top Bottom