Mwelekeo wa Ndoa yangu umefikia pabaya sana

Unaonea huruma watoto wako, wakati hata wewe ni mtoto wa watu.
Kina wakati kuishi na watu wasio sahihi kwetu ni kitanzi cha kurudisha nyuma maendeleo ya uchumi wa familia.
Fika sehemu, fanya maamuzi magumu hakikisha watoto unaishi nao.
Pia angalia sana huyu wa pili mwenye kukujali sana, Siku atakayoingia ndani, utakuja kukuta yeye sasa ndio Lucifer mwana wa yezebeli
 
Aisee nimelia
 
Inawezekana kuna mambo ameyajua/ ameambiwa ndio yanayomfanya awe na mawazo, kwa kipindi hiki cha sasa ambapo mwanamke anaambiwa ambiwa tu kuwa amefungwa na watu wa 'dini' kinawapa shida sana. Kinawafanya usiku wanaamka na presha, wananuna nuna, wanaona wengine wote ni wakosaji. Pengine ameambiwa na wanawake wenzake. Akiwa nje ataonesha tabasamu sana (kisaikolojia mtu anayeonesha maisha yake ni mazuri nje ujue ndani kuna kitu). Hapa ianbidi umuulize vizuri kinachomtatiza, kinachompa shida ya moyo.
.
Upande mwingine ni wewe mwenyewe, inawezekana kuna sehemu ulianza kutetereka kuwa mwanaume wa kumuongoza. Kuna sehemu apo umesema humfuatilii kabisa, kiukweli (haijalishi wanawake wa kisasa wanasemaje) wanawake wanahitaji mtu wa kumuongoza, mtu wa kumuambia hiki hapana, asipopata hayo huishia kuwa na kinyongo kwa mwanaume wake na kuanza kumletea vituko. Kama zamani mlikua mpo vizuri jaribu kukumbuka ni kuanzia wapi mambo yalienda mrama ili alafu angalia nini uliacha kufanya, inawezekana ni kwamba haupati muda naye wa kutosha kiasi akaona unamchukulia poa tu kisa ushamzalisha na hujamtolea mahari.
.
Kujumuisha yote hayo, anza kumuwekea mipaka, mfuatilie kidogo tu kumuonesha kuwa unamjali. Mpe muda ikiwezekana safiri ila muache vizuri, mshirikishe kuwa ungependa mtafute suluhisho ila kama mambo yanaendelea kuwa mabaya, maisha ni mara moja tu mzee, furaha yako ni ya muhimu.
.
Pia unaposema huyo wa nje unatamani ungekua naye, ingekuaje kama huyo wa nje mngefikia kwenye hii tabu uliyonayo na huyo wa ndani, je, ungeenda kutafuta wa nje mwingine au ungetafuta suluhisho?
.
Mi mtazamo wangu, watoto ni jambo jema lakini hawatakiwi kukufunga kufanya maamuzi kwa ajili ya furaha yako, sababu kama huna furaha kwasababu ya watoto watoto watakuaje na furaha kwako?
 
Tafuta sukuhu ya tatizo lako la kupoteza hisia nae na kushindwa kushiriki vema tendo la ndoa naye. Mwanamke kama humfilishi kileleni hawezi kukuheshim. Tafuta tiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…