Si unajua sheria inahusu kucheza na maneno? Ni kama logic. Nilisoma symbolic logic kama somo mwaka mmoja. Tulikuwa na mwalimu fulani Belgian mbobezi sana kwenye logic...baba...ilikuwa kazi. Mfano, unaweza kusema "hata Rais alishalitolea jambo hili ufafanuzi." Atakwambia "So what? That's a fallacy of 'argumentum ad verecundiam' (appeal to authority)". Yaani ulikuwa hupitishi sentensi kwake hajaikosoa. Hata kwa wanasheria ni vivyo hivyo. Siku moja nilikwenda kuulizia kuhusu title ya research yangu, nikakuta ofisini mkuu wa masuala ya research za LLB. Sasa nikaulizia kwa Kiswahili, yeye akajibu kwa Kiingereza. Akaanza kuniuliza maswali. Hujamaliza kujibu, ameshauliza lingine. Unajibu hilo, ameshakwenda kwa lingine, ili mradi tu wewe ushindwe. Baadaye, sijui alijifikiria nini akaanza kuongea kwa utaratibu, na akaona nilikuwa na hoja ya kuuliza nilivyouliza, na akanijibu, na hata akanisindikiza kutoka ofisini mwake. Kwa hiyo, mwanasheria akishaona udhaifu mahali fulani anajibanza hapo, na hutoboi. Kwenye sheria ni hivi: X anaweza kupigwa na kuumizwa na Y. X anaweza kujua kujitetea mahakamani vizuri kuliko Y. Hukumu inaweza kutolewa kwamba X hajampiga wala kumuumiza Y, wakati watu waliona kabisa akimpiga na kumuumiza Y. Katika mazingira fulani sheria inaweza kupindishwa, au hata kama haipindishwi, ushahidi uliotolewa unaweza kumfanya mwenye haki atiwe hatiani, na mwenye hatia aachiwe huru.