Tetesi: Mwendelezo wa Kununua Watumwa: Mbunge wa Simanjiro James Ole Millya Kuhamia CCM

Tetesi: Mwendelezo wa Kununua Watumwa: Mbunge wa Simanjiro James Ole Millya Kuhamia CCM

Status
Not open for further replies.

Zapa RadioFm

Senior Member
Joined
Feb 12, 2016
Posts
112
Reaction score
171
Mbunge wa Simanjiro James Ole Millya,kuhamia Chama cha Mapinduzi muda wowote kuanzia sasa. Millya ni miongoni mwa wabunge wa Upinzani wenye ushawishi kanda ya kaskazini kutokana na uzoefu wa siasa za kanda hiyo.

milia.jpg
 
ooh yeah, i saw it coming...long baaaack....!
Siasa maslahi.

All the best!
 
Tunaenda wapi na hii tabia ya wapinzani wa Tanzania kuhama vyama.
 
Eti kununuliwa!

Kama chama wabunge wake wote hao na madiwani wananunuliwa tafsiri ni kwamba ni chama mfu, na wapiga kura wasimchague yeyote toka chama hicho sababu kesho atanunuliwa.

Lakini ukweli wa mambo ni kwamba hakuna anayenunuliwa, ni kutokana na madhaifu ya ndani ya chama na mazuri ya serikali ndo mana wabunge na madiwani wanaamia huko.

Sasa hizo propaganda za kuwadanganya manyumbu hazikubaliki na walio wengi. Nyie badala ya kurekebisha mapungufu yenu mnapiga propaganda za kudanganya, haisaidii.

Endeleeni kudanganyana
 
Chadema walichagua wagombea wanaonunulika 2015, inatakiwa wawaombe radhi wananchi wa maeneo hayo kwa kuwa walipaswa kuchagua wagombea wasio na tabia hizo
Wa kwanza kuomba radhi ni CCM inatakiwa iwaombe radhi watanzania kwa kuteua Mgombea aliyeshinda na anayetumia fedha vibaya za umma kununua Wabunge, wanachama na viongozi wa vyama vya upinzani
 
Mbunge wa Simanjiro James Ole Millya,kuhamia Chama cha Mapinduzi muda wowote kuanzia sasa. Millya ni miongoni mwa wabunge wa Upinzani wenye ushawishi kanda ya kaskazini kutokana na uzoefu wa siasa za kanda hiyo.

View attachment 669789
Chadema sio mtu ni Taasisi tofauti na CCM kama anataka kuondoka aende tunamtakia safari njema ila asigeuka nyuma
 
Eti kununuliwa!

Kama chama wabunge wake wote hao na madiwani wananunuliwa tafsiri ni kwamba ni chama mfu, na wapiga kura wasimchague yeyote toka chama hicho sababu kesho atanunuliwa.

Lakini ukweli wa mambo ni kwamba hakuna anayenunuliwa, ni kutokana na madhaifu ya ndani ya chama na mazuri ya serikali ndo mana wabunge na madiwani wanaamia huko.

Sasa hizo propaganda za kuwadanganya manyumbu hazikubaliki na walio wengi. Nyie badala ya kurekebisha mapungufu yenu mnapiga propaganda za kudanganya, haisaidii.

Endeleeni kudanganyana
Vipi kuhusu ule ushahidi wa Nassari kule Alumeru unauzungumziaje?
 
Hii kama itakuwa kweli na sio propaganda, basi no mawili tuu yaliyotokea :
1. Ama kweli Lowasa anatimiza kazi aliyotumwa .
2. Ama nguvu za ushawishi wa lowasa zimekwisha.

Kitu kinachoitwa floor trading in Parliamentary politics ni jambo huwa linatokea. Kuna wakati India hilo lilivuma sana.
 
Akiona mauzo yamekamilika aanze mbele asiage amwambie mkewe tu na chadema ipo na itabaki milele!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom