Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,409
- 13,262
Yote kwa yote tunaoumia ni sisi wananchi wa kawaida. Kwani miamala ya manunuzi na gharama za chaguzi za marudio mzigo wote ni wetu sisi. Wanaosema demokrasia ina gharama wao wenyewe hawagharimii bali wanagharimiwa na watu masikini wa nchi hii kutokana na kodi wanazolipa. Hiki kinachofanyika sasa ni gharama za demokrasia za kijinga. Hizi siyo demokrasia wanazozihitaji watu. Bwana machafuko alishatangaza kuwa uchaguzi umekwisha sasa tuchape makazi lakini sasa badala ya kuchapa kazi inakuwa kila mwezi tunafanya chaguzi za marudio za madiwani na wabunge kwasababu wanajiuzulu kwa nyakati tofauti hivyo kila mwezi tutakuwa na chaguzi ndogo lakini ambazo zinatafuna mabilioni ya pesa za masikini wa nchi hii. Kweli kubip na kusukumizwa ni kubaya sana! Kwakuwa pesa zetu wao ndio wanaoamua matumizi yake, waweke siku maalumu yakumaliza manunuzi ili baada ya hapo uchaguzi mdogo uitishwe na ufanyike kwa siku moja na iwe marufuku kurudia chaguzi kwenye kata na majimbo ya "waliojiuzulu"