Mwendokasi zinavituko sana kuna siku nilikuwa ubungo maji dereva alichapwa makofi sana na abiria wenye hasira Kali hadi aligoma endesha...hahaha
Tukio lilikuwa kama ifuatavyo abiria tumejaa kituoni magari yanakuja yanapitiliza huyu dereva yeye alikuja kwa speed kama anapitiliza alafu akasimama alipoweka gari vizuri watu wanajipanga kugombania ingia jamaa wala hakufungua milango akaondoa gari watu walipiga kelele balaa kumbe lengo lake kuwa chora abiria akasogea kidogo mpaka kwenye zebra kasimama anawaangalia watu alafu anacheka akarudisha gari alipofungua mlango tu hahaha kuna mzee wa makamo alimchapa makofi ya hatari sana jamaa alilia akagoma endesha mzee akamwambia sasa ngoja niwapigie maboss zako, ikabidi jamaa aendeshe tu kishingo upande