MwendoKasi Special Thread: (Mikasa na vituko vinavyojiri kwenye mabasi ya Mwendokasi)

MwendoKasi Special Thread: (Mikasa na vituko vinavyojiri kwenye mabasi ya Mwendokasi)

Mwendokasi zinavituko sana kuna siku nilikuwa ubungo maji dereva alichapwa makofi sana na abiria wenye hasira Kali hadi aligoma endesha...hahaha

Tukio lilikuwa kama ifuatavyo abiria tumejaa kituoni magari yanakuja yanapitiliza huyu dereva yeye alikuja kwa speed kama anapitiliza alafu akasimama alipoweka gari vizuri watu wanajipanga kugombania ingia jamaa wala hakufungua milango akaondoa gari watu walipiga kelele balaa kumbe lengo lake kuwa chora abiria akasogea kidogo mpaka kwenye zebra kasimama anawaangalia watu alafu anacheka akarudisha gari alipofungua mlango tu hahaha kuna mzee wa makamo alimchapa makofi ya hatari sana jamaa alilia akagoma endesha mzee akamwambia sasa ngoja niwapigie maboss zako, ikabidi jamaa aendeshe tu kishingo upande
[emoji23] [emoji23] [emoji1]
 
Mwendo kasi inaleta umaskini popote utapopandia ni 650.
Lakini kuna option ya kupanda gari linaloenda sehemu yoyote baadae ukaunganisha huko mbeleeni mf. Unataka kwenda Kimara kutoka Gerezani halafu gari za kimara ukakuta ziko full, hapohapo kuna gari za ubungo kwahiyo unaweza kupanda za Ubungo halafu ukifika Ubungo unashuka ubasubiri ya Kimara ikija unaendelea na safari.
Hicho kitu hakipo kwa daladala za kawaida.
 
Back
Top Bottom