Mwenendo na ukatili wa askari wetu unatafakatisha na kuhuzunisha

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,483
Reaction score
40,130
Hakuna asiyejua kwamba mtawala aliyepo sasa ni mkandamizaji na muuaji dhidi ya raia wake wanaokosoa utendaji wake.

Analitumia jeshi letu kwa ujumla wake kama jeshi lake binafsi. Tumeona baadhi ya wananjeshi wakivikwa sare za polisi wakati wananchi walipotaka kuandamana kupinga utekaji, utesaji na mauaji ya raia.

Jeshi letu limejipa jukumu la kutekekeza kila amri na maagizo ya viongozi wa juu bila kuchakata athari za kijamii na kibinadamu.

Tumesikia shuhuda za wanaotekwa na kuteswa kisha kunusurika namna ambavyo walipelekwa maeneo ya vikosi vyetu kuteswa na kutupwa huko.

Tunashuhudia namna ambayo askari mbele ya kamera wakiwapiga na kuwafanyia ukatili mkubwa wanasiasa wa upinzani.

Matendo haya na ukimya wa viongozi hususan Amiri Jeshi Mkuu, inaleta maana moja kwamba amri zinatoka juu. Juu wapi naamini jibu unalo ndugu msomaji.

Itoshe kusema askari wetu wamefuzu na kuhitimu katika medani za UKATILI DHIDI YA BINADAMU. Wanaweza sasa kukodiwa kama mamluki kwenye maeneo yanayohitaji askari wa kukodiwa. Wanaweza hata kushirikiana na magaidi duniani maana matendo yao hayana utofauti na magaidi.

Natoa hoja
 
Kuna culture inatakiwa ibadilike kwenye hizo taasis kutoka force to service

Bado kuna culture ya kikoloni inaendelea nayo ni kutumia nguvu all the time
 
..hata wakoloni wa kiingereza hawakuwa wakatili kwa Tanu, ukilinganisha na Ccm walivyo wakatili kwa wapinzani.

..kwa mfano, nitajie tukio lolote lile la Mwalimu Nyerere kukamatwa, kudhalilishwa, na kujeruhiwa, kama ilivyotokea kwa Prof Lipumba, Freeman Mbowe, au Tundu Lissu.
 
Kuna culture inatakiwa ibadilike kwenye hizo taasis kutoka force to service

Bado kuna culture ya kikoloni inaendelea nayo ni kutumia nguvu all the time
Hoja yako ni dhaifu, hapo Kenya walishatoka huko kwenye mfumo wa Force na sasa wanatumia service ila mbona utendaji kazi wao ni kama huu wa vyombo vyetu vya Tz! Acheni kuiga kwa nchi za magharibi.
 
Mimi nafikiri serikali iendelee kufanya hivyo hivyo kwa raia ili ukombozi uje kwa haraka

Polisi waendelea kuwapiga wapinzani, wananchi wanaoleta fyoko fyoko
Serikali ya CCM ihakikishe inafanya kila mbinu rushwa, kununua wapinzani, kuwateka, kuwapoteza, kuwatisha ili iendelee kubaki madaraka

Lakini bahati mbaya mwisho wa CCM umefika.
 
Majuzi hapa nilikuwa napiga story na dada yangu mmoja akaniambia nilikuwa siamini ulichoniambia ile March 2021 kuwa CCM ni ile ile .

Baada ya Magufuli kufariki nilisema hata humu hata huyu mama sina imani naye maana ni suala la muda angeonyesha makali yake tu kwa watu na kweli miezi 5 mbele Mbowe akapewa kesi ya ugaidi.

Huyu dada yangu kwa sasa anamuita Samia "Bi Mwenda " na mimi ikabidi nilichukue jina hili na kifupi hana hamu nae na haamini mwanamke anaweza kuwa katili hivi.
 
Back
Top Bottom