Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,264
Tangu Kisutu hadi mahakama kuu nikifuatilia hii kesi ya uhaini nimefikia hitimisho kuwa kinachofanyika ni figisu tu. Lugha ngumu, mabuku makubwa, muda mwingi kupotea, na mavazi yenye madoido mengi, n.k.
Fikiria mtu anajenga hoja na kujenga hadi unaziona lakini watu wanateta kando kisha wanasema wametupilia mbali hoja husika.
Binafsi nimekuwa na kesi mahakamani. Pale kama huna hatia, kuweka wakili ni kupoteza muda na fedha. Kinyume na hapo mbwembwe zote hizo za kisheria lengo lake ni kutetea uhalifu na wahalifu.
Sheria wala sio ngumu kama wanavyotaka tuamini. Sheria maana yake ni kusimamia yaliyo ya haki. Kwamba kuna watu wanaoitwa mahakimu hukaa pale na kutoa maamuzi juu ya mwenendo wa kesi. Sasa ugumu wa kesi huja pale ambapo haki huanza kuporwa kwa njia ya rushwa.
Kinyume chake ni busara, hekima na haki tu ndivyo vinavyohitajika katika kutoa maamuzi na hukumu. Busara na hekima kama aliyotumia Suleiman kwenye kesi ya mtoto.
Ukitata kujua sheria si jambo la kimantiki tazama vile ambavyo hao mahakimu na majaji hupokea maagizo toka juu. Mtu ambaye alisoma na kusoma na kukariri ila mwisho anakuja kupokea maagizo ili kupindisha ukweli.
Ifike muda tuiangalie upya sheria na kuachana na zile mbwembwe nyingi ambazo hazina mashiko zaidi ya kupoteza tu muda